Na Mapuli Misalaba, Shinyanga
Kikundi cha Jamii mpya Mama yangu, Nchi yangu Mkoa
wa Shinyanga kimetoa msaada wa vitu
mbalimbali kwa wanafunzi wa shule ya msingi Buhangija jumuishi kufuatia Bweni la
shule hiyo kutetekea kwa moto Novemba 22 Mwaka huu 2022.
Vitu
vilivyotolewa na kikundi cha Jamii mpya ni pamoja na sabuni, miswaki, dawa ya meno, Dofi, Juice pamoja na Biscut kama hatua ya kusaidia kituo hicho ambacho kinauhitaji
wa vitu mbalimbali baada ya kutokea kwa ajali hiyo.
Akizungumza
wakati wa hafla hiyo mratibu wa kikundi cha Jamii mpya Mkoa wa Shinyanga Bwana Leonard Maige amesema
msaada huo ni sehemu ya kikundi hicho kuwafariji wanafunzi wa shule hiyo baada
ya kupatwa na tukio hilo.
“Tulipokea kwa maskitiko makubwa
tukio lililotokea hapa shuleni na kusababisha Bweni kuungua moto ambapo watoto
watatu walifariki Dunia sisi kama jamii
mpya Mkoa wa Shinyanga tunatoa vitu baadhi vichache kwa ajili ya kuwashika
mkono na sisi tumeguswa na ndiyo maana nimeamua tuje tuwape hiki tulichonacho”.amesema Mratibu Leonard Maige
Akizungumza
baada ya kupokea msaada huo Mwalimu wa shule ya msingi Buhangija Mashinde Daudi
amekishukuru kikundi cha Jamii mpya mama yangu, Nchi yangu kwa kuguswa na tukio
hilo.
“Kwa niamba ya stafu shule ya msingi
Buhangija tunawashukuru sana kikundi cha Jamii mpya kwa kuwa pamoja na hawa
watoto kwa kuguswa kuja kutoa hivi vitu ambavyo vitasaidia kupunguza changamoto”.amesema
Mwalimu Mashinde Daudi
Watu
mbalimbali wameendelea kupeleka msaada wa aina mbalimbali kwa wanafunzi wa Bweni
wa shule ya msingi Buhangija jumuishi kama hatua ya kusaidia mahitaji baada ya
Bweni moja la wanafunzi wa kike kuungua na kuteketeza magodoro, vitanda na
vifaa vya shule.
Jamii mpya ni kundi la kizalendo kwa Taifa, serikali
na chama cha mapinduzi ambacho kinafanya kazi chini ya ofisi ya mkuu wa Mkoa,
mkuu wa Wilaya na wakurugenzi wa Halmashauri kwa kushiriki shughuli mbalimbali
za maendeleo, kijamii, elimu na kuhamasisha vijana na wanawake kuchangamkia fursa
mbalimbali za kiuchumi.
Aidha kikundi cha Jamii mpya kinafanya kazi kupitia
kampeni ya kitaifa ijulikanayo kama MAMA YANGU, NCHI YANGU na kwamba
kilianzishwa Mwaka 2018 chini ya mawaziri, wakuu wa Mikoa na wakurugenzi kwa
lengo la kuunganisha makundi ya vijana, wanawake na wanaume ili kwa pamoja
kushiriki shughuli za uzalishaji mali, uchumi na mambo ya kijamii na kuweza
kumuunga mkono Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu
Hassan.
Mratibu wa kikundi cha Jamii mpya Mkoa wa Shinyanga Bwana Leonard Maige akizungumza kwenye hafla hiyo
Katibu wa kikundi cha Jamii mpya Mama yangu, Nchi yangu Mkoa wa Shinyanga Bi. Selina Leonce Kimola akizungumza kabla ya kukabidhi msaada huo.
Post a Comment