Na Mapuli Misalaba, Shinyanga
Mbunge wa jimbo la Shinyanga Mjini Naibu Waziri wa Nchi ofisi ya Waziri Mkuu kazi,vijana, ajira na wenye ulemavu,Paschal Patrobas katambi leo Desemba 15, 2022 amezungumza na Wananchi wa Jimbo la Shinyanga Mjini akieleza utekelezaji wa ilani ya CCM.
Mbunge huyo amezungumza na Wananchi kupitia Mkutano wa hadhara uliofanyika katika viwanja vya Jeshi la zimamoto Nguzonane Mjini Shinyanga ambapo ameelezea mafanikio yaliyofikiwa katika utekelezaji wa ilani ya Uchaguzi ya Mwaka 2020.
Mh: Katambi amesema miradi mbalimbali iliyokuwa ikitekelezwa katika jimbo la Shinyanga mjini inaendelea vizuri na kwamba baadhi ya miradi imekamilika kwa asilimia mia moja.
Mbunge wa jimbo la Shinyanga Mjini Naibu Waziri wa Nchi ofisi ya Waziri Mkuu kazi,vijana, ajira na wenye ulemavu,Paschal Patrobas katambi ameeleza kuwa ataendelea kushughulikia changamoto zote zilizopo kwenye jimbo la Shinyanga mjini kupitia sekta mbalimbali ikiwemo sekta ya Elimu, afya pamoja na miundombinu.
Amesema ipo mikakati mbalimbali inayolenga kukuza uchumi ikiwa ni pamoja na wananchi wa Jimbo la Shinyanga mjini kunufaika na miradi mbalimbali ambapo amesema hatokubali kuona changamoto zikiendelea kurudisha nyuma maendeleo ya jimbo la Shinyanga.
Aidha Mbunge wa jimbo la Shinyanga Mjini Naibu Waziri wa Nchi ofisi ya Waziri Mkuu kazi,vijana, ajira na wenye ulemavu,Paschal Patrobas katambi ametumia nafsi hiyo kumpongeza Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa ushirikiano wake katika utatuzi wa changamoto zinazowakabili wananchi wa jimbo la Shinyanga mjini.
Mbunge huyo pia aliandaa Maadhimisho ya Siku Maalumu ya Kumpongeza Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan iliyopewa jina la ‘SAMIA DAY’ yakiongozwa na Kauli Mbiu ‘ASANTE MAMA TUMEKUELEWA NA KAZI IENDELEE’.
Kwa upande wake Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi Mkoa wa Shinyanga Mh. Mabala Mlolwa amesema chama hicho kitaendelea kusimamia utekelezaji wa miradi mbalimbali kupitia ilani ya chama hicho ili kutatua kero za wananchi.
Mwenyekiti huyo wa CCM Mkoa wa Shinyanga Mh: Mabala amempongeza Mwenyekiti wa CCM Taifa ambaye pia ni Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa kuendelea kuwajari wananchi kwa kutatua changamoto zinazowakabil.
Naye mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Sophia Mjema amewaomba wananachi wa Mkoa wa Shinyanga kuendelea kuiunga mkono serikali ya awali ya sita inayoongozwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tazania Dkt. Samia Suluhu Hassan
Mbunge wa jimbo la Shinyanga Mjini Naibu Waziri wa Nchi ofisi ya Waziri Mkuu kazi,vijana, ajira na wenye ulemavu,Paschal Patrobas katambi akizungumza na wananchi kwenye mkutano wa hadhara mjini Shinyanga.

Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi Mkoa wa Shinyanga Mh. Mabala Mlolwa akizungumza na wananchi kwenye mkutano wa hadhara.
Mkurugenzi wa Mamlaka ya Maji safi
na Usafi wa Mazingira Shinyanga (SHUWASA) Mhandisi Yusuph akizungumza kwenye maadhimisho
ya Samia Day.
Katibu mwenezi wa CCM Wilaya ya Shinyanga mjini Said Bwanga akizungumza kwenye mkutano huo.
Mbele ni baadhi ya viongozi wa kikundi cha Jamii mpya Mama yangu, Nchi yangu Mkoa wa Shinyanga wakienda eneo la mkutano wa hadhara kushirikia maadhimisho ya SAMIA DAY Desemba 15,2022.

Mbunge wa jimbo la Shinyanga Mjini Naibu Waziri wa Nchi ofisi ya Waziri Mkuu kazi,vijana, ajira na wenye ulemavu,Paschal Patrobas katambi awali wakati akiingia kwenye eneo la mkutano akiwa ameambatana na viongozi mbalimbali wa chama.
Upande wa kulia ni Mbunge wa jimbo la Shinyanga Mjini Naibu Waziri wa Nchi ofisi ya Waziri Mkuu kazi,vijana, ajira na wenye ulemavu,Paschal Patrobas katamb akiwa na mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Shinyanga Mh: Mabala Mlolwa.
Nyuma ni viongozi wa kikundi cha Jamii mpya Mkoa wa Shinyanga wakishiriki maadhimisho ya siku ya SAMIA DAY katika viwanja vya Zima moto Nguzonane mjini Shinyanga.




Upande wa kulia ni Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Sophia Mjema akiteta jambo la Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Shinyanga Mh: Mabala Mlolwa.






Baadhi ya viongozi wa kikundi cha Jamii mpya Mamam yangu, Nchi yangu wakiwa katika picha ya pamoja na viongozi wa CCM kwenye ofisi za CCM Wilaya ya Shinyanga mjini.
Post a Comment