" MGOMBEA UDIWANI WA ACT WAZALENDO KATA YA MWAMALILI ASIMAMA KUOMBA KURA KWA WANANCHI

MGOMBEA UDIWANI WA ACT WAZALENDO KATA YA MWAMALILI ASIMAMA KUOMBA KURA KWA WANANCHI

Na Mapuli Misalaba, Shinyanga

Chama cha ACT  Wazalendo kimezindua kampeni za uchaguzi mdogo wa nafasi ya udiwani kata ya Mwamalili ambapo kimewaomba  wananchi wa eneo hilo kukichagua chama hicho ili kiweze kuleta mzukumo wa maendeleo katika kata hiyo.

Akizindua kampeni hizo kupitia mkutano wa hadhara katika kijiji cha Seseko kata ya Mwamalili mjumbe wa Halmashauri kuu ya ACT Wazalendo Taifa Bwana Shilungushela Nyangaki amewaomba wakazi wa kata hiyo kumchagua mgombea wa ACT Wazalendo ili kumpa nafasi ya kuwa muwakilishi wao kwenye baraza la madiwani la Halmashauri ya Manispaa ya Shinyanga.

Bwana Shilungushela amemuombea kura mgombea wa chama hicho akisema iwapo atachaguliwa ataweka msukumo wa kuleta maendeleo.

“Ukiwa hapa Seseko utafikiri siyo Manispaa ni kwa sababu ya kukosa mtetezi makini kwa sababu mapato ya mjini yanatakiwa yaje huku mboreshewe miundombinu maisha yatengamae unatakiwa ufikie umeme hapa kuweni waelewa changamkieni fursa hii iliyojitokeza mjaribu kubadilisha uongozi huyu Joseph Machiya anatosha”.amesema Shilungushela

 Akizungumza katika kampeni hiyo mgombea wa nafasi ya udiwani kata ya mwamalili  kupitia chama cha ACT Wazalendo Bwana Joseph Yunja Machiya amewaomba kura wananchi wa kata hiyo ili aweze kushughulikia changamoto zinazowakabili.

“Nawaomba sana vijana, akina Baba, akiwa Maba na wazee mnipe kura tarehe 17 na jira langu nila kwaza tu kwenye karatasi ukiona tu picha yangu weka vema kuna kero nyingi sana za hapa kata ya Mwamalili endapo mkinipa kura nitahakikisha mnapata umeme na maji yanakuja lakini pia changamoto zote mtanituma na nitazifikisha kingine nitahakikisha kila baada ya miezi mitatu nafanya mkutano wa hadhara”.amesema Joseph Machiya

Aidha viongozi mbalimbali wa chama cha ACT Wazalendo  ngazi ya Mkoa na wilaya wametumia nafasi hiyo kuwaomba wananchi wa kata ya Mwamalili kumchagua mgombea wao Joseph Machiya  katika nafasi ya udiwani.

Wakati huo huo baadhi ya wananchi wa kata ya Mwamalili wamesema wanahitaji kupata mwakilishi mwenye sifa za kiongozi bora katika nafasi hiyo ya udiwani.

Uchaguzi huo mdogo wa nafasi ya udiwani kata ya Mwamalili unafanyika kuziba pengo la aliyekuwa diwani wa kata hiyo Paulo Machela ambaye alifariki Dunia Mwanzoni mwa Mwaka huu 2022.mjumbe wa Halmashauri kuu ya ACT Wazalendo Taifa Bwana Shilungushela Nyangaki akiomba kura kwa wananchi.Katibu wa ACT Wazalendo Mkoa wa Shinyanga Merikioli Sebastian akiwaomba wananchi wa kata ya Mwamalili kumchagua mgombea wao joseph MachiyaKatibu wa  chama cha ACT Wazalendo Jimbo la Shinyanga mjini Saimon Tungu akiwaomba wananchi kumchagua Joseph Machiya kuwa diwani wa kata hiyo.Katibu wa Ngome ya vijana kupitia chama cha ACT Wazalendo  Mkoa wa Shinyanga Juster Denis akiwaomba kura za ndiyo wananchi wa kata hiyo waweze kumpigia Joseph Machiya 




Post a Comment

Previous Post Next Post