" WALIMU WA SEKONDARI WASHEREHEKEA MEI MOSI KWA KISHINDO SHINYANGA

WALIMU WA SEKONDARI WASHEREHEKEA MEI MOSI KWA KISHINDO SHINYANGA


Viongozi wakiongozwa na Afisa Elimu Mkoa, Naibu Meya, Katibu wa Mbunge, Mdhibiti Mkuu wa Ubora pamoja na Mwl. Makoye wakikata keki kwa pamoja kuadhimisha umoja wa walimu katika sherehe za Mei Mosi.


Walimu wa shule za sekondari katika Manispaa ya Shinyanga wameadhimisha Siku ya Wafanyakazi Duniani (Mei Mosi) kwa sherehe maalum iliyofanyika Mei 1, 2026 katika viwanja vya Family Park, ikiwa na lengo la kuwatambua na kuwapongeza kwa mchango wao katika sekta ya elimu.

Sherehe hiyo iliandaliwa na Afisa Elimu Sekondari wa Manispaa ya Shinyanga, Mwl. Richard Makoye, ambaye pia ni mfanyakazi bora wa mwaka 2026 katika manispaa hiyo.

Kauli mbiu ya sherehe hiyo ni “Sisi Wote ni Watumishi Bora” iliwakutanisha walimu mbalimbali ambapo walipata fursa ya kula, kunywa na kuburudika kupitia muziki, burudani za moja kwa moja pamoja na shughuli mbalimbali ikiwemo upigaji picha za pamoja.

Miongoni mwa matukio yaliyovutia zaidi ni mashindano ya kumtafuta Miss Teacher na Mr Teacher, ambapo washindi waliibuka na zawadi nono. Katika mashindano hayo, taji la Miss Teacher lilinyakuliwa na Madam Nurah Kamuntu ambaye  ni Mkuu wa Shule ya Sekondari Shinyanga Girls, huku Mr Teacher akiibuka kuwa Mwalimu Seif Juma wa Shule ya Sekondari Busulwa ambaye pia ni Katibu wa Michezo wa Manispaa ya Shinyanga.

Timu ya majaji wa mashindano hayo iliongozwa na Afisa Michezo wa Manispaa ya Shinyanga, Bw. Arnold Lukiza.

Mgeni rasmi katika sherehe hiyo alikuwa Afisa Elimu wa Mkoa wa Shinyanga, Mwl. Samson A. Hango, ambaye aliwapongeza walimu kwa kazi kubwa wanayoifanya na kuwataka kuendelea kujituma ili kuinua kiwango cha elimu kwa wanafunzi wa Tanzania. Aidha, aliwapongeza viongozi wa elimu kwa ubunifu wa kuandaa tukio hilo.

Kwa upande wake, Naibu Meya wa Manispaa ya Shinyanga, Mhe. Pendo Sawa, alisema tukio hilo ni la kipekee kwani limewawezesha walimu kukutana na kusherehekea mafanikio yao, akipendekeza liwe linafanyika kila mwaka.

Wageni wengine wa heshima waliohudhuria ni pamoja na Katibu wa Mbunge, Bw. Samwel Jackson, Mdhibiti Mkuu wa Ubora wa Elimu Mkoa Bi. Edith Kaijage, Kaimu Mkurugenzi wa Manispaa Charles Luchagula, madiwani pamoja na viongozi mbalimbali.

Afisa Elimu Sekondari wa Manispaa ya Shinyanga, Mwl. Richard Makoye, ambaye pia ni mfanyakazi bora wa mwaka 2026 katika manispaa hiyo alipongezwa kwa maandalizi mazuri ya tukio hilo lililowaleta pamoja walimu katika mazingira ya furaha na mshikamano.

Afisa Elimu wa Mkoa wa Shinyanga, Mwl. Samson A. Hango, akizungumza na walimu wakati wa maadhimisho ya Mei Mosi yaliyofanyika Family Park, Shinyanga.






 SHY TALENT FILMS - CONTENT YA MWISHO DRAMA

🥃🍶 TUMIA VINYWAJI BORA VYA KAMPUNI YA EAST AFRICAN SPIRITS – BEI RAFIKI, LADHA SAFI BILA HARUFU MBAYA

  • Wasiliana nasi:
    📍 East African Spirits (T) Ltd
    📞 +255 767 650 806 | +255 652 096 254

Post a Comment

Previous Post Next Post