Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi,Patrobas Katambi ametoa ufafanuzi juu ya zoezi nzima la Urejeshaji na Ufungaji wa Kambi ya Wakimbizi wa Burundi nchini ambao walikua wanahifadhiwa katika Kambi ya Nduta iliyoko mkoani Kigoma.
Waziri Katambi ametoa ufafanuzi huo wakati wa Mahojiano na Mwandishi wa Habari ambapo alielezea utaratibu wote ulivyofuatwa ikiwemo vikao kadhaa vya pande tatu ikiwemo Serikali ya Tanzania,Serikali ya Burundi na Shirika la Kuhudumia Wakimbizi Duniani(UNHCR).
“Tumekaa vikao vya pamoja na makubaliano kulingana na sheria zinavyoelekeza,kunakua na uratibu wa hatua kwa hatua na kuna zile sababu zilizofanya wakimbie zisiwepo tena na moja ya sababu ni kutokuwepo kwa vita katika nchi husika lakini pia kusiwe na matishio ya kiusalama ambayo yanapelekea matishio ya vifo au mateso makali.” amesema Waziri Katambi
“Sisi Serikali ya Tanzania tumehakikisha mazingira hatarishi katika nchi yao wanayorudi yako Salama,Rais wa Burundi Mheshimiwa Evariste Ndayishimiye pamoja na Balozi wa Burundi hapa nchini wamethibitisha kwamba nchi yao iko salama na tayari maeneo ya kufikia yameandaliwa na huduma zao muhimu ikiwemo afya,elimu,maji na ustawi wao kwenye nchi hiyo.” aliongeza Waziri Katambi
Ni takribani miaka 10 Serikali ya Tanzania imehifadhi Wakimbizi hao wa Burundi katika Kambi ya Nduta ambayo hadi kufungwa kwake rasmi tarehe 30 Aprili,2026 ilikua na jumla ya Wakimbizi 165,394 ambapo katika Mkutano wa 26 wa Pande Tatu;Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,Serikali ya Burundi na Shirika la Kuhudumia Wakimbizi Duniani(UNHCR) uliofanyika tarehe 28 Novemba,2025 jijini Dar es Salaam uliazimia na pande zote tatu kutiliana saini makubaliano ya kuanza Urejeshaji wa Wakimbizi hao ambapo hatua iliyofuatia ni kufungwa kwa kambi hiyo.
SHY TALENT FILMS - CONTENT YA MWISHO DRAMA
🥃🍶 TUMIA VINYWAJI BORA VYA KAMPUNI YA EAST AFRICAN SPIRITS – BEI RAFIKI, LADHA SAFI BILA HARUFU MBAYA
Wasiliana nasi:
📍 East African Spirits (T) Ltd
📞 +255 767 650 806 | +255 652 096 254
Post a Comment