Na Mapuli Kitina Misalaba
Mkurugenzi wa mashindano ya NIACHEKONA CUP 2026, Paul
Daud Augustino maarufu MC NIACHEKONA, amewaalika wananchi, wadau wa michezo na
wapenda soka kutoka maeneo mbalimbali kujitokeza kwa wingi kushuhudia kilele
cha mashindano hayo kitakachofanyika kesho Jumanne, Juni 23, 2026, katika
Uwanja wa Mwabenda, Kata ya Solwa, Halmashauri ya Wilaya ya Shinyanga.
Akizungumza kuelekea mchezo wa fainali, MC NIACHEKONA
amesema shughuli za siku hiyo zitaanza mapema kwa mchezo wa kusaka mshindi wa
tatu utakaozikutanisha Bulige FC na Duara FC (Mwabenda) kuanzia saa nane kamili
mchana.
Amesema baada ya mchezo huo kutakuwa na burudani
mbalimbali zitakazotolewa na vikundi na wasanii tofauti, ikiwemo Kundi la
Dancers Kambi ya Nyani, kikundi cha tarumbeta pamoja na wasanii wa nyimbo za
asili, kwa lengo la kuwapa burudani wananchi watakaohudhuria siku hiyo.
MC NIACHEKONA amesema saa kumi kamili jioni atawasili
mgeni rasmi wa mashindano hayo, Mhe. Masalu Nyese, Diwani wa Kata ya
Mwakitolyo, ambaye amealikwa kutokana na mchango wake katika maendeleo ya
michezo na vijana.
Ameeleza kuwa uwepo wa mgeni rasmi utatoa fursa ya
kuzungumza na vijana na wadau wa michezo kuhusu namna ya kuendeleza vipaji,
kuhamasisha ushirikiano pamoja na kufikisha ujumbe kwa serikali na wadau
wengine ili kuendelea kuimarisha sekta ya michezo.
Kwa mujibu wa MC NIACHEKONA, shughuli za itifaki
zitasimamiwa na MC Dizzo, ambaye atakuwa na jukumu la kumkaribisha mgeni rasmi
pamoja na wageni wengine waalikwa kabla ya kuanza kwa mchezo wa fainali.
Mchezo wa fainali utawakutanisha Ufukunyungu FC kutoka
Manispaa ya Shinyanga na Kashishi FC kutoka Kata ya Solwa, timu mbili
zilizofanikiwa kuzishinda timu nyingine 20 na kufuzu hatua ya mwisho kati ya
timu 22 zilizoshiriki mashindano hayo mwaka huu.
Ameongeza kuwa mshindi wa kwanza atazawadiwa Kombe
pamoja na shilingi milioni 1.2, huku mshindi wa pili akipata shilingi laki 6 na
mshindi wa tatu shilingi laki 3.
Pia kutakuwa na tuzo mbalimbali za binafsi na timu,
ambapo mchezaji bora, golikipa bora na mfungaji bora kila mmoja atapata
shilingi elfu 50,000. Aidha, timu yenye nidhamu bora nayo itatunukiwa zawadi
maalum kwa kutambua umuhimu wa kuzingatia maadili na sheria za mashindano.
MC NIACHEKONA amesema mgeni rasmi ameziarika timu zote
zilizoshiriki mashindano hayo ili kuhudhuria siku ya fainali kwa ajili ya
kupata hamasa na mafunzo yatakayosaidia maendeleo ya michezo katika maeneo yao.
Mashindano ya NIACHEKONA CUP 2026 yameandaliwa na Paul
Daud Augustino maarufu MC NIACHEKONA kwa ufadhili wa Shirika la Lushu
Foundation, yakilenga kuibua vipaji vya vijana, kukuza michezo na kuimarisha
mshikamano wa jamii.
Kwa huduma za MC, matangazo na ushereheshaji wa
matukio mbalimbali, wasiliana na MC NIACHEKONA kupitia namba 0757 267 738.
MC NIACHEKONA , akizungumza na watanzania kupitia Misalaba Media.
SHY TALENT FILMS - CONTENT YA MWISHO DRAMA
🥃🍶 TUMIA VINYWAJI BORA VYA KAMPUNI YA EAST AFRICAN SPIRITS – BEI RAFIKI, LADHA SAFI BILA HARUFU MBAYA
Wasiliana nasi:
📍 East African Spirits (T) Ltd
📞 +255 767 650 806 | +255 652 096 254

Post a Comment