" UFUKUNYUNGU FC YATINGA FAINALI BAADA YA KUIFUNGA DUARA FC KWA PENATI

UFUKUNYUNGU FC YATINGA FAINALI BAADA YA KUIFUNGA DUARA FC KWA PENATI

Ndani ya dakika 90 za mchezo huo, timu hizo zilitoka sare ya goli 1-1. Ufukunyungu FC ndiyo ilikuwa ya kwanza kupata bao katika kipindi cha kwanza kabla ya Duara FC kusawazisha kipindi cha pili na kufanya mchezo huo kumalizika kwa sare.

Matokeo hayo yalizifanya timu hizo kwenda kwenye mikwaju ya penati ambapo Ufukunyungu FC ilionyesha utulivu mkubwa na kufanikiwa kushinda kwa penalti 5-4, ushindi ulioihakikishia nafasi ya kucheza fainali ya mashindano hayo.

Kwa ushindi huo, Ufukunyungu FC imekuwa timu ya kwanza kufuzu fainali na sasa inamsubiri mshindi wa mchezo wa kesho wa nusu fainali kati ya Bulige FC na Kashishi FC ili kujua mpinzani wake wa mwisho katika mbio za ubingwa.

Kwa upande wa Duara FC, bado ina nafasi ya kumaliza katika nafasi ya tatu, ambapo itacheza na timu itakayofungwa katika mchezo wa kesho wa nusu fainali.

Akizungumza baada ya mchezo huo, Katibu wa Kamati ya Mashindano, Sambayi Jilya, ametangaza kuwa mchezo wa pili wa nusu fainali utachezwa kesho ukizikutanisha Bulige FC na Kashishi FC katika pambano la kusaka tiketi ya pili ya kucheza fainali.

Aidha, ratiba ya fainali tayari imetangazwa ambapo siku ya Jumanne, Juni 23, 2026, kutakuwa na mchezo wa kusaka mshindi wa tatu kuanzia saa nane mchana, huku mchezo wa fainali ukitarajiwa kuanza saa kumi jioni.

Mashindano ya NIACHEKONA CUP 2026 yameandaliwa na Paul Daud Augustino maarufu MC NIACHEKONA kwa ufadhili wa Shirika la Lushu Foundation, yakilenga kuibua vipaji vya vijana, kukuza michezo na kuimarisha mshikamano wa jamii.

Kwa huduma za MC, matangazo na ushereheshaji wa matukio mbalimbali, wasiliana na MC NIACHEKONA kupitia namba 0757 267 738.

Kikosi cha Duara FC na sabu.


 SHY TALENT FILMS - CONTENT YA MWISHO DRAMA

🥃🍶 TUMIA VINYWAJI BORA VYA KAMPUNI YA EAST AFRICAN SPIRITS – BEI RAFIKI, LADHA SAFI BILA HARUFU MBAYA

  • Wasiliana nasi:
    📍 East African Spirits (T) Ltd
    📞 +255 767 650 806 | +255 652 096 254

Post a Comment

Previous Post Next Post