" RATIBA YA ROBO FAINALI NIACHEKONA CUP 2026 YATANGAZWA RASMI

RATIBA YA ROBO FAINALI NIACHEKONA CUP 2026 YATANGAZWA RASMI

Kamati ya Mashindano ya NIACHEKONA CUP 2026 imetangaza rasmi ratiba ya michezo ya hatua ya robo fainali itakayokutanisha timu nane zilizofanikiwa kufuzu hatua hiyo baada ya kuonyesha kiwango kizuri katika michezo iliyopita.

Kwa mujibu wa ratiba hiyo, mchezo wa kwanza wa robo fainali utachezwa leo Juni 13, 2026 ambapo Songambele Mhangu FC kutoka Kata ya Salawe, Halmashauri ya Wilaya ya Shinyanga itamenyana na Ufukunyungu FC kutoka Kata ya Ngokolo, Manispaa ya Shinyanga.

Mnamo Juni 14, 2026, Duara FC Mwabenda itashuka dimbani kuivaa Mawemiru FC katika pambano jingine la kusaka tiketi ya kutinga hatua ya nusu fainali.

Mchezo wa tatu wa robo fainali utachezwa Juni 15, 2026 na kuzikutanisha Nyandolwa FC dhidi ya Bulige Stars FC, huku kila timu ikisaka nafasi ya kuendelea mbele katika mashindano hayo.

Hatua ya robo fainali itahitimishwa Juni 16, 2026 kwa mchezo kati ya Kashishi FC na Shilabela FC, pambano ambalo linatarajiwa kuwa na ushindani mkubwa kutokana na kiwango walichoonyesha timu hizo katika hatua zilizopita.

Mashindano ya NIACHEKONA CUP 2026 yanaendelea katika Uwanja wa Mwabenda, Kata ya Solwa Mkoani Shinyanga, yakiwa yameandaliwa na Paul Daud Augustino maarufu MC NIACHEKONA kwa ufadhili wa Shirika la Lushu Foundation, yakilenga kuibua vipaji vya vijana, kukuza michezo na kuimarisha mshikamano wa jamii.

Kwa mawasiliano ya shughuli mbalimbali za kijamii, michezo, matangazo na ushereheshaji wa matukio, wasiliana na MC NIACHEKONA kupitia namba 0757 267 738.

RATIBA KWA UFUPI

🏆 13/06/2026

  • Songambele Mhangu FC vs Ufukunyungu Shy Mjini FC

🏆 14/06/2026

  • Duara FC vs Mawemiru FC

🏆 15/06/2026

  • Nyandolwa FC vs Bulige Stars FC

🏆 16/06/2026

  • Kashishi FC vs Shilabela FC

Uwanja: Mwabenda, Kata ya Solwa
Muda: Saa kumi Jioni

 SHY TALENT FILMS - CONTENT YA MWISHO DRAMA

🥃🍶 TUMIA VINYWAJI BORA VYA KAMPUNI YA EAST AFRICAN SPIRITS – BEI RAFIKI, LADHA SAFI BILA HARUFU MBAYA

  • Wasiliana nasi:
    📍 East African Spirits (T) Ltd
    📞 +255 767 650 806 | +255 652 096 254

Post a Comment

Previous Post Next Post