Askofu Johnson Japheth Chinyong'ole akitoa mahubiri na nasaha mbalimbali kwa Mchungaji Kanoni Jackson Daudi Iseke pamoja na waumini waliohudhuria ibada hiyo.Na Mapuli Kitina Misalaba
Kanisa la Anglikana Solwa Kashishi la Dayosisi ya
Shinyanga limefanya ibada maalum ya kumstaafisha Mchungaji Kanoni Jackson Daudi
Iseke baada ya kulitumikia Kanisa kwa miaka mingi katika nafasi mbalimbali za
uongozi wa kiroho.
Ibada hiyo iliyofanyika Juni 7, 2026 katika Kanisa la
Anglikana Solwa Kashishi ilihudhuriwa na Askofu wa Dayosisi ya Shinyanga,
Mhashamu Johnson Japheth Chinyong'ole, viongozi mbalimbali wa Kanisa, waumini
pamoja na familia ya Mchungaji Kanoni Jackson Iseke.
Ibada hiyo iliongozwa na Katibu wa Dayosisi ya
Shinyanga, Noel Bahati, huku historia fupi ya maisha na utumishi wa Mchungaji
Kanoni Jackson Iseke ikisomwa na Shemasi Jefta Stanford Riniga.
Akihubiri katika ibada hiyo, Askofu Johnson Japheth
Chinyong'ole alimpongeza Mchungaji Kanoni Jackson Iseke kwa uaminifu wake
katika kulitumikia Kanisa na kumweleza kuwa kustaafu kwake ni mwisho wa nafasi
ya kiuongozi lakini si mwisho wa utumishi wake kwa Mungu.
Askofu Chinyong'ole alisema kuwa Kanisa bado
linahitaji hekima, ushauri na uzoefu wa viongozi waliolitumikia kwa muda mrefu,
hivyo Mchungaji Iseke ataendelea kuwa mshauri muhimu kwa Kanisa, viongozi na
waumini.
"Umeacha nafasi ya uongozi kwa mujibu wa taratibu
za Kanisa, lakini bado wewe ni mtumishi wa Mungu. Tunaamini utaendelea kuwa
mshauri na mfano bora kwa kizazi kinachoendelea na kazi ya Injili,"
alisema Askofu Chinyong'ole.
Kwa upande wake, Mchungaji Kanoni Jackson Iseke pamoja
na familia yake walimshukuru Mungu kwa kuwawezesha kufika hatua hiyo ya ustaafu
salama na kuwashukuru viongozi wa Kanisa, waumini, ndugu na marafiki kwa
ushirikiano walioupata katika kipindi chote cha utumishi wake.
Baadhi ya viongozi na waumini wa Kanisa hilo waliopata
nafasi ya kuzungumza walieleza kuwa Mchungaji Iseke ameacha alama kubwa katika
maendeleo ya Kanisa la Solwa Kashishi, wakibainisha kuwa wakati anaanza
kulitumikia eneo hilo hakukuwa na maendeleo makubwa ya miundombinu ya Kanisa,
lakini kwa ushirikiano wa waumini na uongozi wake, hatua mbalimbali za
maendeleo ikiwemo ujenzi wa Kanisa zimefanikiwa.
Kwa mujibu wa historia iliyosomwa, Mchungaji Kanoni
Jackson Daudi Iseke alizaliwa Julai 1, 1954 katika Kitongoji cha Nhwiga, Kijiji
cha Kabiga, Kata ya Kakola. Katika maisha yake ya utumishi amehudumu katika
nafasi mbalimbali ikiwemo Mhazini wa Parishi ya Kakola, Mwinjilisti wa Parishi
ya Nyang'ombe, Shemasi, Kasisi na baadaye kuhamishiwa Parishi ya Solwa Kashishi
mwaka 2015.
Mwaka 2017 alipandishwa Daraja la Ukanoni na Askofu
Johnson Japheth Chinyong'ole kutokana na mchango wake katika kuhubiri Injili na
kuimarisha huduma za Kanisa.
Ibada hiyo ilihitimishwa kwa sala za shukrani na
kumuombea Mchungaji Kanoni Jackson Daudi Iseke afya njema, amani na baraka za
Mungu katika maisha yake ya ustaafu huku akiendelea kuwa nguzo ya ushauri kwa
Kanisa na jamii kwa ujumla.
Askofu Johnson Japheth Chinyong'ole akitoa mahubiri na nasaha mbalimbali kwa Mchungaji Kanoni Jackson Daudi Iseke pamoja na waumini waliohudhuria ibada hiyo.
Katibu wa Dayosisi ya Shinyanga, Noel Bahati, akiongoza ibada maalum ya kustaafu kwa Mchungaji Kanoni Jackson Daudi Iseke.
Mchungaji Kanoni Jackson Daudi Iseke (wa kwanza kushoto) akizungumza mbele ya waumini, viongozi wa Kanisa na familia yake wakati wa ibada maalum ya kustaafu iliyofanyika katika Kanisa la Anglikana Solwa Kashishi, Dayosisi ya Shinyanga
Katibu wa Dayosisi ya Shinyanga, Noel Bahati, akiongoza ibada maalum ya kustaafu kwa Mchungaji Kanoni Jackson Daudi Iseke.
Askofu wa Dayosisi ya Shinyanga, Johnson Japheth Chinyong'ole, akiongoza ibada ya ubatizo wa mtoto iliyofanyika sambamba na ibada ya kustaafu kwa Mchungaji Kanoni Jackson Daudi Iseke.
Wazazi na walezi wa mtoto aliyebatizwa wakishiriki ibada ya ubatizo katika Kanisa la Anglikana Solwa Kashishi.
Askofu wa Dayosisi ya Shinyanga, Johnson Japheth Chinyong'ole, akiongoza ibada ya ubatizo wa mtoto iliyofanyika sambamba na ibada ya kustaafu kwa Mchungaji Kanoni Jackson Daudi Iseke.
Askofu wa Dayosisi ya Shinyanga, Johnson Japheth Chinyong'ole, akiongoza ibada ya ubatizo wa mtoto iliyofanyika sambamba na ibada ya kustaafu kwa Mchungaji Kanoni Jackson Daudi Iseke.
Askofu wa Dayosisi ya Shinyanga, Johnson Japheth Chinyong'ole, akiongoza ibada ya ubatizo wa mtoto iliyofanyika sambamba na ibada ya kustaafu kwa Mchungaji Kanoni Jackson Daudi Iseke.
Askofu wa Dayosisi ya Shinyanga, Johnson Japheth Chinyong'ole, akiongoza ibada ya ubatizo wa mtoto iliyofanyika sambamba na ibada ya kustaafu kwa Mchungaji Kanoni Jackson Daudi Iseke.
Waumini wa Kanisa la Anglikana Solwa Kashishi wakifuatilia ibada maalum ya kustaafu kwa Mchungaji Kanoni Jackson Daudi Iseke.
Waumini wa Kanisa la Anglikana Solwa Kashishi wakifuatilia ibada maalum ya kustaafu kwa Mchungaji Kanoni Jackson Daudi Iseke.
Waumini wa Kanisa la Anglikana Solwa Kashishi wakifuatilia ibada maalum ya kustaafu kwa Mchungaji Kanoni Jackson Daudi Iseke.
Waumini wa Kanisa la Anglikana Solwa Kashishi wakifuatilia ibada maalum ya kustaafu kwa Mchungaji Kanoni Jackson Daudi Iseke.
Waumini wa Kanisa la Anglikana Solwa Kashishi wakifuatilia ibada maalum ya kustaafu kwa Mchungaji Kanoni Jackson Daudi Iseke.
Waumini wa Kanisa la Anglikana Solwa Kashishi wakifuatilia ibada maalum ya kustaafu kwa Mchungaji Kanoni Jackson Daudi Iseke.
Waumini wa Kanisa la Anglikana Solwa Kashishi wakifuatilia ibada maalum ya kustaafu kwa Mchungaji Kanoni Jackson Daudi Iseke.
Katibu wa Dayosisi ya Shinyanga, Noel Bahati, akiongoza ibada maalum ya kustaafu kwa Mchungaji Kanoni Jackson Daudi Iseke.
Kwaya ya Kanisa la Anglikana Solwa Kashishi ikitoa ujumbe wa kiroho kupitia nyimbo mbalimbali wakati wa ibada maalum ya kustaafu kwa Mchungaji Kanoni Jackson Daudi Iseke.

Katibu wa Dayosisi ya Shinyanga (wa kwanza kushoto aliyeketi), Askofu wa Dayosisi ya Shinyanga Johnson Japheth Chinyong'ole (wa pili kushoto), Mchungaji Kanoni Jackson Daudi Iseke aliyestaafu (wa tatu kushoto) pamoja na mke wake Mama Mary Mabula Nhomange wakipiga picha ya kumbukumbu na viongozi wa Kanisa, waumini na familia baada ya ibada maalum ya kustaafu iliyofanyika katika Kanisa la Anglikana Solwa Kashishi.
Askofu Johnson Japheth Chinyong'ole, viongozi wa Kanisa, Mchungaji Kanoni Jackson Daudi Iseke pamoja na familia ya mchungaji Iseke wakipiga picha ya kumbukumbu baada ya kumalizika kwa ibada hiyo.SHY TALENT FILMS - CONTENT YA MWISHO DRAMA

Post a Comment