" ASKOFU CHINYONG'OLE: AMANI NI MSINGI WA MAENDELEO YA TAIFA, TUILINDE KWA PAMOJA

ASKOFU CHINYONG'OLE: AMANI NI MSINGI WA MAENDELEO YA TAIFA, TUILINDE KWA PAMOJA

Na Mapuli Kitina Misalaba

Askofu wa Kanisa la Anglikana Dayosisi ya Shinyanga, Johnson Japheth Chinyong'ole, amewataka Watanzania kuendelea kuilinda na kuitunza amani ya nchi kwa kujiepusha na vitendo vinavyoweza kusababisha migogoro, chuki na mifarakano katika jamii.

Askofu Chinyong'ole ametoa wito huo wakati wa ibada maalum ya kumstaafisha Mchungaji Kanoni Jackson Daudi Iseke baada ya kulitumikia Kanisa kwa miaka mingi, na kwamba imefanyika katika Kanisa la Anglikana Solwa Kashishi, akisisitiza kuwa amani ni msingi muhimu wa maendeleo ya taifa na ustawi wa wananchi.

Amesema kuwa bila amani hakuna maendeleo yanayoweza kupatikana, hivyo kila mwananchi ana wajibu wa kuhakikisha anashiriki katika kuijenga na kuilinda amani iliyopo nchini.

Aidha, amewahimiza viongozi wa dini na wananchi kutumia maneno ya upendo, hekima na maridhiano katika kushughulikia tofauti za mawazo ili kudumisha mshikamano miongoni mwa Watanzania.

Baadhi ya waumini waliohudhuria ibada hiyo akiwemo James Nangi, Elizabeth Jackson, Paul Yohana na Eliana Charles wameeleza umuhimu wa kuendelea kuombea taifa na viongozi wake, wakisema kuwa amani iliyopo nchini imewezesha wananchi kufanya shughuli zao za maendeleo kwa utulivu.

Wamesema kuwa jamii inapaswa kuendelea kuhubiri upendo, umoja na mshikamano ili kuimarisha amani iliyojengwa kwa miaka mingi nchini Tanzania.

Waumini hao wamewataka vijana kujiepusha na vitendo vya vurugu na badala yake kujikita katika shughuli za uzalishaji mali na maendeleo ya taifa, huku wakisisitiza kuwa amani ni nguzo muhimu ya maendeleo endelevu.

Wamesema kuwa ushirikiano kati ya viongozi wa dini, Serikali na wananchi ni muhimu katika kuendelea kuimarisha umoja wa kitaifa na kudumisha sifa ya Tanzania kuwa kisiwa cha amani barani Afrika.

Askofu Johnson Japheth Chinyong'ole akitoa mahubiri na nasaha mbalimbali

 SHY TALENT FILMS - CONTENT YA MWISHO DRAMA

🥃🍶 TUMIA VINYWAJI BORA VYA KAMPUNI YA EAST AFRICAN SPIRITS – BEI RAFIKI, LADHA SAFI BILA HARUFU MBAYA

  • Wasiliana nasi:
    📍 East African Spirits (T) Ltd
    📞 +255 767 650 806 | +255 652 096 254

Post a Comment

Previous Post Next Post