Na, Egidia Vedasto, Misalaba Media, Arusha ._Kongamano la Kitaifa Lachagiza Uwajibikaji na Uwazi Sekta ya Umma_Serikali imezitaka taasisi za umma kuimarisha mifumo ya uwajibikaji, uwazi na udhibiti wa ndani ili kukabiliana na vitendo vya udanganyifu vinavyoathiri matumizi sahihi ya rasilimali za taifa na utoaji wa huduma kwa wananchi.Akifungua Kongamano la Uhamasishaji wa Kupambana na Udanganyifu katika Sekta ya Umma (Public Sector Fraud Awareness Forum) Jijini Arusha, Naibu Gavana wa Benki Kuu ya Tanzania (BoT), Dkt. Rahma Salim Mahfoudh, amesema mapambano dhidi ya udanganyifu yanahitaji ushirikiano wa karibu kati ya taasisi za umma, sekta binafsi na wataalamu wa uchunguzi, huku akisisitiza matumizi ya teknolojia za kisasa na mifumo madhubuti ya udhibiti ili kulinda rasilimali za taifa."Udanganyifu ni moja ya kikwazo kikubwa kinachozorotesha maendeleo katika jamii, ni wazi kwamba watumishi wadanganyifu na Wala rushwa ni sababu kubwa inayokwamisha jitihada za serikali katika kuharakisha maendeleo ya watu wake" amesema Dkt. Rahma.Kwa upande wake Rais wa ACFE Tanzania Chapter, Aly Mbaruku Juma, amesema taasisi hiyo imeendelea kufanya tafiti za kitaalamu kuhusu mwenendo wa udanganyifu katika sekta mbalimbali kwa lengo la kusaidia taasisi kubaini maeneo yenye vihatarishi na kuimarisha mifumo ya usimamizi na uadilifu.Katika namna hiyohiyo Mkaguzi Mkuu wa Ndani kutoka Ofisi ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG), Kenneth Nindie amesema kasi ya maendeleo ya teknolojia imeongeza ufanisi katika usimamizi wa mifumo ya kifedha, lakini pia imeibua mbinu mpya za udanganyifu zinazohitaji taasisi kuwekeza zaidi katika usalama wa taarifa na mafunzo ya wataalamu.Kongamano hilo la siku tano limewakutanisha viongozi wa taasisi za umma, wakaguzi wa ndani, wataalamu wa uchunguzi wa udanganyifu, usimamizi wa hatari na fedha kutoka maeneo mbalimbali nchini kujadili mikakati ya kuimarisha uwajibikaji, uwazi na ulinzi wa rasilimali za umma.Hata hivyo Washiriki wanatarajiwa kutoka na mapendekezo yatakayosaidia kuimarisha vita dhidi ya udanganyifu, kuongeza uwajibikaji wa taasisi za umma na kuboresha usimamizi wa rasilimali kwa manufaa ya maendeleo ya taifa.SHY TALENT FILMS - CONTENT YA MWISHO DRAMA
🥃🍶 TUMIA VINYWAJI BORA VYA KAMPUNI YA EAST AFRICAN SPIRITS – BEI RAFIKI, LADHA SAFI BILA HARUFU MBAYA
Wasiliana nasi:
📍 East African Spirits (T) Ltd
📞 +255 767 650 806 | +255 652 096 254
Post a Comment