Na Mapuli Kitina Misalaba
Timu ya Songambele Mhangu FC imefanikiwa kutinga hatua
ya robo fainali ya mashindano ya NIACHEKONA CUP 2026 baada ya kuibuka na
ushindi wa bao 1-0 dhidi ya Duara FC katika mchezo mkali uliochezwa leo Jumatatu
Juni 8, 2026 katika uwanja wa Mwabenda, Kata ya Solwa, Halmashauri ya Wilaya ya
Shinyanga.
Bao pekee la ushindi katika mchezo huo lilifungwa na Masanja
Kabelele katika dakika ya sita ya mchezo, bao ambalo lilidumu hadi filimbi ya
mwisho na kuipa Songambele Mhangu FC tiketi ya kusonga mbele katika hatua
inayofuata ya mashindano hayo.
Licha ya Duara FC kufanya jitihada mbalimbali za
kutafuta bao la kusawazisha, safu ya ulinzi ya Songambele Mhangu FC ilisimama
imara na kufanikiwa kulinda ushindi huo muhimu.
Kutokana na matokeo hayo, safari ya Duara FC katika
mashindano ya NIACHEKONA CUP 2026 imefikia tamati. Viongozi wa timu hiyo
wameushukuru uongozi wa mashindano pamoja na mwandaaji kwa kuwapa nafasi ya
kushiriki, huku wakikiri kuwa hawakufanikiwa kufikia malengo waliyojiwekea
msimu huu.
Akizungumza baada ya mchezo huo, Katibu wa Mashindano
ya NIACHEKONA CUP ametangaza ratiba ya mchezo wa kesho ambapo Home Boys FC
kutoka Kata ya Solwa watamenyana na Ufukunyungu FC kutoka Kata ya Ngokolo,
Manispaa ya Shinyanga, katika pambano linalotarajiwa kuwa na ushindani mkubwa.
Kwa upande wake, Mkurugenzi wa Mashindano hayo, Bwana
Paul Daud Augustino maarufu MC NIACHEKONA, amewashukuru wananchi na wadau wa
michezo kwa kuendelea kujitokeza kwa wingi kufuatilia mechi mbalimbali
zinazochezwa kila siku katika uwanja wa Mwabenda.
Amesema mwitikio mkubwa wa wananchi unaonesha kuwa
mashindano hayo yamekubalika na yanaendelea kutimiza lengo la kuibua vipaji vya
vijana pamoja na kutoa burudani kwa jamii.
Aidha, amewahimiza wananchi kuendelea kujitokeza kwa
wingi kushuhudia vipaji vya vijana na watoto wao wanaoshiriki katika mashindano
hayo.
Sambamba na hilo, MC NIACHEKONA ameielekeza Kamati ya
Mashindano kuendelea kusimamia kwa umakini kanuni na taratibu zilizowekwa ili
kuhakikisha mashindano yanaendeshwa kwa haki, amani na nidhamu.
Amesisitiza kuwa hatua stahiki zichukuliwe dhidi ya
timu au watu watakaokiuka kanuni za mashindano hayo ili kulinda hadhi ya ligi
na kuhakikisha wananchi wanaendelea kupata burudani katika mazingira ya amani
na utulivu.
Mashindano ya NIACHEKONA CUP 2026 yameandaliwa na
Bwana Paul Daud Augustino maarufu MC NIACHEKONA kwa ufadhili wa shirika la Lushu
Foundation, yakiwa na lengo la kuibua vipaji vya vijana, kuimarisha mshikamano
wa jamii na kukuza michezo katika Mkoa wa Shinyanga na maeneo jirani.
Kwa huduma za ushereheshaji wa matukio mbalimbali,
matangazo na burudani, MC NIACHEKONA anapatikana kupitia namba 0757 267 738.
Kikosi cha Songambele Mhangu FC.
Kikosi cha Duara FC.
Mkurugenzi wa Mashindano ya NIACHEKONA CUP 2026, Bwana Paul Daud Augustino maarufu MC NIACHEKONA, akizungumza na wananchi kabla ya kuanza kwa mchezo wa leo huku akiwashukuru kwa kuendelea kujitokeza kwa wingi kushuhudia mashindano hayo.
Bwana Paul Daud Augustino (MC NIACHEKONA), mwandaaji na mkurugenzi wa mashindano ya NIACHEKONA CUP, akitoa maelekezo na kuwataka wadau wa michezo kuendelea kudumisha amani, mshikamano na ushirikiano kabla ya kuanza kwa mchezo wa leo.
Paul Daud Augustino maarufu MC NIACHEKONA akizungumza kabla ya mchezo wa leo, ambapo amewapongeza wananchi kwa mwitikio mkubwa wa kufuatilia mashindano hayo tangu yalipoanza.
Mkurugenzi wa Mashindano ya NIACHEKONA CUP 2026, Bwana Paul Daud Augustino maarufu MC NIACHEKONA, akizungumza na wananchi na wadau wa michezo kabla ya kuanza kwa mchezo wa leo katika Uwanja wa Mwabenda, huku akiwashukuru kwa kuendelea kuunga mkono mashindano hayo yanayolenga kuibua vipaji vya vijana na kuimarisha mshikamano wa jamii.
Wachezaji wakioneshana uwezo mkubwa katika pambano la kusaka nafasi ya kutinga hatua inayofuata ya mashindano ya NIACHEKONA CUP 2026.
Ushindani mkubwa ukiendelea uwanjani huku kila timu ikisaka bao la ushindi mbele ya mashabiki waliojitokeza kwa wingi.
Burudani ya soka ikiendelea katika Uwanja wa Mwabenda huku vijana wakionesha vipaji vya hali ya juu.
Viongozi wa mashindano na wadau wa michezo ikiwepo Diwani wa kata ya Solwa wakifuatilia kwa karibu mechi ya leo katika NIACHEKONA CUP 2026, mashindano yanayoendelea kuvutia wananchi kutoka maeneo mbalimbali.

Maelfu ya wananchi wanaendelea kujitokeza kila siku katika Uwanja wa Mwabenda kushuhudia burudani ya soka, kuunga mkono vipaji vya vijana na kufuatilia kwa karibu mashindano ya NIACHEKONA CUP 2026.
Wananchi wa Solwa na maeneo jirani wakiendelea kujitokeza kwa wingi kufuatilia vipaji vya vijana kupitia mashindano hayo.

Mashabiki wakifurahia mchezo wa leo huku wakionesha mapenzi makubwa kwa michezo na vipaji vya vijana.

Maelfu ya wananchi wanaendelea kujitokeza kila siku katika Uwanja wa Mwabenda kushuhudia burudani ya soka, kuunga mkono vipaji vya vijana na kufuatilia kwa karibu mashindano ya NIACHEKONA CUP 2026.SHY TALENT FILMS - CONTENT YA MWISHO DRAMA
🥃🍶 TUMIA VINYWAJI BORA VYA KAMPUNI YA EAST AFRICAN SPIRITS – BEI RAFIKI, LADHA SAFI BILA HARUFU MBAYA
Wasiliana nasi:
📍 East African Spirits (T) Ltd
📞 +255 767 650 806 | +255 652 096 254

Post a Comment