Timu ya Community Development imeibuka bingwa wa
mashindano ya Interclass katika Chuo cha Serikali za Mitaa (CSGM) Kampasi ya
Shinyanga baada ya kuichapa Finance mabao 4-0 katika mchezo wa fainali
uliochezwa kwa ushindani mkubwa.
Fainali hiyo ilihudhuriwa na mgeni rasmi Samwel
Jackson, Katibu wa Mbunge wa Jimbo la Shinyanga Mjini, ambaye aliwapongeza
wanafunzi kwa kujitokeza kushiriki michezo na kudumisha umoja, ushirikiano na
nidhamu kupitia mashindano hayo.
Akizungumza katika hafla ya kufunga mashindano hayo,
Samwel Jackson alisema michezo ni nyenzo muhimu ya kujenga afya, kuibua vipaji
na kuwaunganisha vijana, huku akiwataka wanafunzi kuendelea kutumia michezo
kama sehemu ya kujenga mahusiano mema na kujiandaa kwa majukumu ya maendeleo ya
jamii.
Katika mchezo huo wa fainali, Community Development
ilionyesha ubora mkubwa uwanjani kwa kutawala mchezo na kufanikiwa kuibuka na
ushindi mnono wa mabao manne bila majibu dhidi ya Finance, matokeo
yaliyoiwezesha kutwaa ubingwa wa mashindano hayo ya Interclass.
Mashindano hayo yaliyoandaliwa kwa ushirikiano wa
Wizara ya Habari na Wizara ya Michezo ndani ya chuo hicho yalihusisha michezo
mbalimbali ikiwemo mpira wa miguu, netiboli na riadha, yakilenga kukuza vipaji
na kuimarisha mshikamano miongoni mwa wanafunzi.
Katika hayo Mshindi wa mpira wa miguu alipokea zawadi
ya mbuzi mmoja, huku washindi wa michezo mingine na watu binafsi waliofanya
vizuri wakitunukiwa zawadi mbalimbali.
Wanafunzi na wadau waliohudhuria fainali hiyo
walieleza kufurahishwa na kiwango cha ushindani kilichoonyeshwa na timu zote,
huku wakiipongeza Community Development kwa kuonyesha kiwango bora na kustahili
ubingwa huo.
Matokeo ya Fainali
Community Development 4-0 Finance

mgeni rasmi Samwel Jackson, Katibu wa Mbunge wa Jimbo la Shinyanga Mjini akizungumza.
Mwenyekiti wa mtaa wa Miti mirefu Nassor Mokhe.











SHY TALENT FILMS - CONTENT YA MWISHO DRAMA
🥃🍶 TUMIA VINYWAJI BORA VYA KAMPUNI YA EAST AFRICAN SPIRITS – BEI RAFIKI, LADHA SAFI BILA HARUFU MBAYA
Wasiliana nasi:
📍 East African Spirits (T) Ltd
📞 +255 767 650 806 | +255 652 096 254

































Post a Comment