Abiria wametakiwa kushiriki kikamilifu katika kuzuia usafirishaji wa watoto wanaopelekwa kufanyishwa kazi za ndani au kufanyiwa vitendo vingine vya unyonyaji kwa kutoa taarifa wanapobaini mazingira yanayotia shaka.Rai hiyo imetolewa na Sajenti David Ndimila, Askari Polisi wa Kikosi cha Usalama Barabarani Mkoa wa Shinyanga, alipokuwa akitoa elimu kwa abiria katika Stendi ya Mabasi ya Mkoa wa Shinyanga (Ibinzamata).Amesema kila mwananchi ana wajibu wa kuwa macho na kutoa taarifa kwa Jeshi la Polisi au mamlaka husika endapo atabaini mtoto anayesafirishwa katika mazingira yanayotia shaka, akisisitiza kuwa taarifa za mapema zinaweza kuokoa maisha na mustakabali wa mtoto.Sajenti Ndimila ametaja baadhi ya viashiria vinavyoweza kuashiria mtoto yuko hatarini, ikiwemo mtoto anayesafiri peke yake bila mzazi au mlezi anayejulikana, mtoto mwenye umri wa kwenda shule anayesafiri bila maelezo ya kuridhisha kuhusu safari yake, mtoto asiyejua anakoelekea au sababu ya safari yake, mtu mzima anayemjibia mtoto maswali yote badala yake, pamoja na mtoto kutokuwa na nyaraka muhimu au mzazi/mlezi kushindwa kuthibitisha uhusiano wake na mtoto.
SHY TALENT FILMS - CONTENT YA MWISHO DRAMA
🥃🍶 TUMIA VINYWAJI BORA VYA KAMPUNI YA EAST AFRICAN SPIRITS – BEI RAFIKI, LADHA SAFI BILA HARUFU MBAYA
Wasiliana nasi:
📍 East African Spirits (T) Ltd
📞 +255 767 650 806 | +255 652 096 254


Post a Comment