Timu ya Kashishi FC imefanikiwa kutinga hatua ya
fainali ya mashindano ya NIACHEKONA CUP 2026 baada ya kuibuka na ushindi wa
goli 1-0 dhidi ya Bulige FC katika mchezo wa nusu fainali uliochezwa leo Juni
19, 2026, kwenye Uwanja wa Mwabenda, Kata ya Solwa, Halmashauri ya Wilaya ya
Shinyanga.
Mchezo huo uliokuwa na ushindani mkubwa uliamuliwa na
bao pekee lililoipa Kashishi FC ushindi muhimu na kuihakikishia nafasi ya
kucheza fainali ya mashindano hayo, huku safari ya Bulige FC ya kuwania ubingwa
ikifikia tamati.
Kwa ushindi huo, Kashishi FC imeungana na Ufukunyungu
FC, ambayo tayari ilifuzu fainali baada ya kuiondoa Duara FC kwa mikwaju ya
penati katika mchezo wa kwanza wa nusu fainali.
Akizungumza baada ya mchezo huo, Mwenyekiti wa Kamati
ya NIACHEKONA CUP, Silas Elias Kadaso, ametangaza kuwa mchezo wa fainali
utafanyika Jumanne, Juni 23, 2026, katika Uwanja wa Mwabenda.
Amesema kabla ya mchezo wa fainali kutachezwa mchezo
wa kusaka mshindi wa tatu kati ya Duara FC na Bulige FC, huku baadaye
Ufukunyungu FC na Kashishi FC wakishuka dimbani kupambania ubingwa wa
NIACHEKONA CUP 2026.
Mashindano ya NIACHEKONA CUP 2026 yameandaliwa na Paul
Daud Augustino maarufu MC NIACHEKONA kwa ufadhili wa Shirika la Lushu
Foundation, yakilenga kuibua vipaji vya vijana, kukuza michezo na kuimarisha
mshikamano wa jamii.
Kwa huduma za MC, matangazo na ushereheshaji wa
matukio mbalimbali, wasiliana na MC NIACHEKONA kupitia namba 0757 267 738.
Kikosi cha Bulige FC.
Wachezaji wa Kashishi FC na Bulige FC wakipambana kusaka tiketi ya kucheza fainali ya NIACHEKONA CUP 2026.
Viongozi wa mashindano na wadau wa michezo wakifuatilia kwa karibu mchezo wa nusu fainali kati ya Kashishi FC na Bulige FC.
Wananchi kutoka maeneo mbalimbali wakijitokeza kwa wingi kushuhudia hatua ya nusu fainali ya NIACHEKONA CUP 2026.
Wananchi kutoka maeneo mbalimbali wakijitokeza kwa wingi kushuhudia hatua ya nusu fainali ya NIACHEKONA CUP 2026.
SHY TALENT FILMS - CONTENT YA MWISHO DRAMA
🥃🍶 TUMIA VINYWAJI BORA VYA KAMPUNI YA EAST AFRICAN SPIRITS – BEI RAFIKI, LADHA SAFI BILA HARUFU MBAYA
Wasiliana nasi:
📍 East African Spirits (T) Ltd
📞 +255 767 650 806 | +255 652 096 254






































Post a Comment