Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Dkt. Samia Suluhu Hassan, amewataka viongozi wote wa Mahakama nchini kuendelea kusimamia nidhamu na uwajibikaji wa hali ya juu katika maeneo yao ya kazi.
Amesisitiza kuwa usimamizi huo ni muhimu sana ili kuhakikisha kuwa wananchi wanapata haki zao kwa wakati unaostahili, kwa heshima inayotakiwa, na kwa mujibu wa sheria za nchi.
Rais Dkt. Samia ameyasema hayo leo tarehe 19 Juni, 2026, akiwa Ikulu ya Dar es Salaam, wakati wa hafla rasmi ya kumuapisha Dkt. John Anthony Jingu kuwa Mtendaji Mkuu wa Mahakama ya Tanzania.
Katika hotuba yake, ameitaka Mahakama ya Tanzania kuendelea kusimamia kwa ukaribu masuala ya haki, nidhamu, uwajibikaji pamoja na maadili mema katika utoaji haki, lengo likiwa ni kujenga na kuwa na mfumo imara wa utoaji wa haki kote nchini.
Aidha amebainisha kuwa Serikali itaendelea kuwezesha Muhimili huo wa Mahakama kwa kuupatia mifumo, miundombinu na rasilimali watu ili kuongeza ufanisi na kuboresha utoaji wa haki na huduma za Mahakama nchini.
Katika hatua nyingine ya hafla hiyo, Rais Dkt. Samia amemtaka Mtendaji Mkuu mpya, Dkt. Jingu, kuendeleza kazi nzuri na ya mfano iliyofanywa na mtangulizi wake, Prof. Elisante Ole Gabriel, ambaye kwa sasa amestaafu.
Rais ametoa shukrani zake za dhati kwa Prof. Gabriel kwa namna alivyosimamia kikamilifu maboresho ya kiutendaji ndani ya Mahakama na kufanikiwa kuacha misingi mizuri na imara inayostahili kuendelezwa.
Aidha, Rais Dkt. Samia amempongeza Jaji Mkuu wa Tanzania, Mhe. George Mcheche Masaju, kwa kuendelea kuisimamia vyema Mahakama kwa ufanisi mkubwa na kwa kuzingatia maadili, hatua ambazo zimesaidia kwa kiasi kikubwa kuimarisha utendaji na hadhi ya Muhimili huo ndani ya mfumo mzima wa haki nchini.
SHY TALENT FILMS - CONTENT YA MWISHO DRAMA
🥃🍶 TUMIA VINYWAJI BORA VYA KAMPUNI YA EAST AFRICAN SPIRITS – BEI RAFIKI, LADHA SAFI BILA HARUFU MBAYA
Wasiliana nasi:
📍 East African Spirits (T) Ltd
📞 +255 767 650 806 | +255 652 096 254

Post a Comment