
Na Stella Herman,Shinyanga
Vijana wametakiwa kujiepusha na vitendo vinavyochochea uvunjifu wa amani na kuacha kutumika kwa maslahi ya watu wachache wanaolenga kuvuruga utulivu wa nchi badala yake wametakiwa kuwa walinzi wa amani, umoja na mshikamano pamoja na kukemea maovu katika jamii.
Wito huo umetolewa na Mwenyekiti wa Jumuiya ya Maridhiano na Amani Mkoa wa Shinyanga (JMAT), Shehe Hamis Balilusa, wakati akizungumza katika mkutano wa Jeshi la Jadi Sungusungu uliofanyika Kata ya Jana, Wilaya ya Kahama mkoani Shinyanga
Shehe Balilusa amesema amani ndiyo msingi wa maendeleo ya taifa, akisisitiza kuwa bila kuwepo kwa amani hakuna shughuli za kijamii wala za kiuchumi zinazoweza kufanyika kwa ufanisi.
"Vijana ni nguvu ya taifa msikubali kutumika kuvuruga amani ya nchi badala yake, simameni kuilinda, kuimarisha umoja na kushirikiana na vyombo vya dola katika kukemea vitendo vya uhalifu," amesema

Kwa upande wake, Kamanda wa Jeshi la Jadi Sungusungu Mkoa wa Shinyanga, John Kadama amewataka Sungusungu kutekeleza majukumu yao kwa kuzingatia sheria, kanuni na taratibu za nchi ili kuhakikisha haki inatendeka na wananchi wanaendelea kuwa na imani na jeshi hilo.
Amesema viongozi wa zamani wa sungusungu wanapochanguliwa walikuwa wanakwenda kuangalia sungusungu inaendaje lakini viongozi wa sasa wanapochaguliwa wanaanza kutunisha mabega hawataki kujua misingi ya sungusungu,tunasema hakuna kujichukulia sheria mkononi zingatieni sheria za nchi na kusimamia ulinzi na amani inaendelea kutawala.
Naye Kamanda wa Jeshi la Polisi Mkoa wa Shinyanga, Janeth Magomi, amesema pamoja na mafanikio yanayopatikana katika kudhibiti uhalifu, bado mkoa huo unakabiliwa na changamoto za ukatili wa kijinsia dhidi ya wanawake na watoto pamoja na migogoro ya ardhi.
Amesema bado watoto wanafanyiwa ukatili wanabakwa,wanapigwa na kunyanyaswa pamoja na ukatili kwa wanawake ni mambo ambayo wanaendelea kuitaka Jamii iachane na vitendo hivyo huku akiwataka sungusungu kufuata sheria na taratibu ili kulinda amani na utulivu.


SHY TALENT FILMS - CONTENT YA MWISHO DRAMA
🥃🍶 TUMIA VINYWAJI BORA VYA KAMPUNI YA EAST AFRICAN SPIRITS – BEI RAFIKI, LADHA SAFI BILA HARUFU MBAYA
Wasiliana nasi:
📍 East African Spirits (T) Ltd
📞 +255 767 650 806 | +255 652 096 254





Post a Comment