Na Mapuli Misalaba, Shinyanga
Mkuu wa
Magereza Mkoa wa Shinyanga kamishna msaidizi wa Magereza Josephine Semwenda amesema
Miaka 61 ya uhuru wa Tanganyika, watanzania waongeze juhudi katika kazi kama
kielelezo cha kuunga mkono dhamira ya
serikali inayolenga kuwa na Taifa lenye uchumi imara.
Amesema
mafanikio mbalimbali yaliyopo yametokana na mifumo thabiti iliyowekezwa, ikiwemo kufanya kazi halali kwa juhudi na
maarifa ili kukuza uchumi wa mtu mmoja mmoja na Taifa kwa ujumla.
Ameyasema
hayo leo wakati akizungumza na Misalaba Blog ofisini kwake kuelekea siku ya
Uhuru wa Tanganyika kesho Disemba 09, ambapo amesema mafanikio yanayoonekana
hivi sasa iwe ni kichocheo cha watanzania wote, kuongeza juhudi na maarifa
katika kazi na shughuli mbalimbali za kiuchumi ikiwemo Biashara, Kilimo na
ujasiliamali.
“Tunafanya jambo jema sana tunapokumbuka siku yetu ya uhuru na tunafanya
kila Mwaka ili kuenzi siku yetu ya uhuru kwanza tunafura lakini pili
tunarithisha kizazi chetu watoto wetu, wajukuu wetu wajue kwamba kumbe Nchi
yetu tulipataga uhuru siku furani”.amesema RPO Semwenda
“Nawashauri watanzania wenzangu tufanye kazi kwa bidii tumuunge mkono
Rais wetu Dkt. Samia Suluhu Hassan maana anafanya kazi sana, anahangaika sana
kutuletea pesa ametuletea ajira basi mtu unapopata ajira fanya kazi kwa tija na
ufanisi lakini pia tufanye kazi kwa kuepuka rushwa tufanye kazi kwa haki
tukifanya hivyo tutakuwa tumemuunga mkono Rais Mama yetu Dkt. Samia Suluhu Hassan.amesema RPO wa
Shinyanga Semwenda
RPO Semwenda amesema Miaka
61 ya uhuru Tanzania licha ya changamoto
kadhaa zilizopo lakini kwa kiwango kikubwa, Nchi imepiga hatua za mafanikio katika sekta mbalimbali ikiwemo sekta
ya uchukuzi hasa katika eneo la uboreshwaji wa miundombinu.
Mkuu
huyo wa Magereza Mkoa wa Shinyanga RPO Semwenda amesema taasisi hiyo
itaadhimisha siku ya uhuru wa Tanganyika kwa kushiriki shughuli mbalimbali za
kijamii ikiwemo usafi wa Mazingira.
Post a Comment