Na Mapuli Misalaba, Shinyanga
Paroko wa parokia ya Mwadui Padre Michel Msabila
amewakumbusha wazazi na walezi kushirikiana na walimu katika malezi ya watoto
shuleni ili waweze kukua katika mazingira ya uadilifu zaidi.
Ametoa mafundisho hayo wakati akihubiri kwenye
adhimisho la misa takatifu ya kumshukuru Mungu kwa ajili ya wanafunzi wahitimu wa
shule ya awali ya St. Mary’s day care iliyofanyika kwenye kanisa la Msalaba
Mtakatifu Parokia ya Mwadui,Wilayani kishapu Mkoani Shinyanga
Amewasisitiza wazazi na
walezi kuwekeza kwenye elimu ya watoto wao kama msingi wa kuwaandaa ili waweze
kukabiliana na mazingira ya Dunia ya sasa inayotaka wasomi.
Padre Msabila ambaye pia ni meneja wa shule hiyo amewataka
wanafunzi wahitimu kuongeza juhudi za kujifunza ikiwa ni pamoja na kuwaheshimu
walimu, wazazi na walezi ili kufikia malengo waliyokusudia
Akizungumza Mkuu wa shule ya awali St. Mary’s day
care Deusdedith Malale amesema Mwaka huu 2022 shule imefanya mahafali ya 24 tangu kuanzishwa
kwake ambapo wanafunzi 36 wamehitimu
masomo yao ya awali.
Aidha mkuu huyo wa shule amesema shule hiyo inatoa mafunzo ya dini kwa
nadharia na vitendo kama chanzo cha maarifa na kutoa elimu bora hivyo amewaomba
wazazi na walezi kupeleka watoto wao katika shule hiyo ili waweze kukua katika
misingi yenye maadili yanayompendeza Mungu.
Kwa upande wao baadhi ya watoto wahitimu katika shule
ya awali St. Mary’s day care centre Mwaka
huu 2022 wamemshukuru Mungu kwa kuhitimu huku wakitoa ahadi zao juu ya elimu
yao kuwa wataendeleza juhudi zao ili kuimarika zaidi kitaaluma.
Post a Comment