" CCM SHINYANGA YAZINDUA KAMPENI ZA UCHAGUZI MDOGO MWAMALILI , MABALA AMSIMAMISHA MDIMI KUELEZA VIPAUMBELE VYAKE.

CCM SHINYANGA YAZINDUA KAMPENI ZA UCHAGUZI MDOGO MWAMALILI , MABALA AMSIMAMISHA MDIMI KUELEZA VIPAUMBELE VYAKE.

Na Mapuli Misalaba, Shinyanga

Chama cha Mapinduzi CCM Wilaya ya Shinyanga Mjini  kimezindua kampeini za uchaguzi mdogo wa nafasi ya udiwani katika kata ya Mwamalili,Jimbo la Uchaguzi la Shinyanga Mjini.

Akizindua kampeni hizo Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Shinyanga Bwana Mabala Mlolwa amewaomba wakazi wa kata hiyo kumchagua mgombea wa CCM Bwana James Mdimi ili aweze kuwasaidia  kutatua changamoto zilizopo katika kata hiyo.

Mwenyekiti huyo amesema iwapo Mdimi atachaguliwa atatumia nafasi yake kushirikiana na viongozi wengine wa chama na serikali kuhakikisha ilani ya uchaguzi inatekelezwa kikamilifu.

“Wana Mwamalili wakiwemo wa Bushola na vijiji vingine niwaombe sana siku ya Jumamosi mkampigie kura Mdimi mtakuwa mmeenda vizuri niwaombe mjitokeze kwa wingi  kwenda kupiga  kura na kura hakuna kwingine zote tumpigie Mdimi”.amesema Mlolwa

“Mdimi ni mgombea wa chama cha mapinduzi atasimamia ilani ya chama ambayo imeainishwa mambo yapi  ya kufanya yamo Mdimi atashirikiana na wenzake madiwani kuhakisha Mwamalili mahitaji yenu mnayoyataka yanakuja kwa uharaka zaidi”.amesema Mwenyekiti wa CCM Mkoa Mabala

Akizungumza katika kampeni hiyo mgombea wa nafasi ya udiwani kata ya mwamalili  Bwana James Mdimi  amewaomba wananchi kumchagua ili aweze kutatua changamoto zilizopo, ambapo amevitaja vipaumbele vyake iwapo atachaguliwa,kuwa ni pamoja na kushughulikia changamoto ya umeme na Maji.

“Mimi ni mwenyeji wa hapa Geographia ya kata ya Mwamalili naifahamu vizuri sana kwahiyo najua Bushola kuna shida gani, Seseko kuna shida gani na Mwamalili kuna shida gani hapa Bushola shida kubwa ni maji ya Victoria lakini pia umeme na vipaumbele vyangu ni maji, umeme, elimu na afya”.amesema Mdimi

Mstahiki Meya wa Manispaa ya Shinyanga Mheshimiwa Elias Ramadhan Masumbuko akiwawakilisha madiwani wengine amewaomba wakazi wa kata ya Mwamalili kumchagua James Mdimi  katika nafasi ya udiwani kata ya Mwalili ili aweze kushughulikia changamoto zilizopo.

Aidha viongozi mbalimbali wa ngazi ya Mkoa na wilaya wametumia nafasi hiyo kuwaomba wananchi wa kata ya Mwamalili kumchagua James Mdimi   katika nafasi ya udiwani kata hiyo.

Kwa upande wao baadhi ya wananchi wa kata ya Mwamalili wamesema wanahitaji mgombea mwenye sifa za uongozi ambaye ataweza kuishnikiza serikali kutatua changamoto na kero zilizopo hali itakayochangia ustawi na maendeleo ya wananchi.

Uchaguzi huo mdogo wa nafasi ya udiwani katika kata ya Mwamalili unafanyika kuziba pengo la aliyekuwa diwani wa kata hiyo Paulo Machela ambaye alifariki Dunia Mwanzoni mwa Mwaka huu 2022.

 

Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Shinyanga Bwana Mabala Mlolwa akizungumza kwenye kampeni kijiji cha Bushola kata ya Mwamalili.Mgombea wa nafasi ya udiwani kata ya mwamalili  Bwana James Mdimi akipandishwa jukwaani kwa ajili ya kuzungumza na wakazi wa kata ya Mwamalili. Katibu mwenezi wa CCM Wilaya ya Shinyanga mjini Bwana Said Bwanga akizungumza kwenye kampeni hiyo.




Post a Comment

Previous Post Next Post