Na Elisha Petro, Shinyanga
Klabu ya Yanga imeibuka na ushindi wa magoli 8 - 0
dhidi ya Kurugenzi kutoka Mkoa wa Simiyu katika raundi ya pili ya michuano ya
Azam Sports (FA) mchezo uliofanyika katika uwanja wa Benjamin Mkapa Jijini Dar
es Salaam.
Katika mchezo huo Clement Mzize amefanikiwa kufunga
magoli 4 na kuandika rekodi ya kufunga goli la mapema zaidi sekunde ya 22 ndani
ya msimu huu 2022/2023 katika mashindano ya FA magoli mengine amefunga dakika
8, 41 na dakika 45).
Yusuph Athuman akitokea benchi kuchukua nafasi ya
Mzize, amefunga magoli mawili dakika ya 79 na 85 wakati David Bryson akifunga
goli dakika ya 77 huku Jefta John Mchezaji wa Kurugenzi akijifunga dakika ya 6.
Aidha mchezo huo ni mchezo wa mwisho kwa kocha mkuu
wa timu hiyo Mohamed Nasreddine Nabi kutumikia adhabu ya kufungiwa kutokuwa
sehemu ya benchi la ufundi kwa michezo mitatu baada ya kujibizana na waamuzi
katika mchezo wa ligi kuu dhidi ya Ihefu Fc.
Klabu ya Yanga ambao ni mabingwa watetezi wa kombe
hilo msimu uliopita 2021/2022 wamefanikiwa kutinga raundi ya 32.
Post a Comment