Na Stela Paul Shinyanga
Wazazi
na walezi wamehimizwa kutekeleza na kusimamia vyema majukumu yao ya msingi kwa
watoto wanaosoma shule za Msingi na Sekondari ikiwa ni pamoja na kuhakikisha
watoto wanapata chakula shuleni ili kuongeza ufaulu pamoja na kutokomeza vitendo vya ukatili wa
kijinsia vinavyofanywa dhidi yao..
Wito
huo umetolewa Disemba 10,2022 na
Kaimu Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Kishapu Mhe. Andason Mandia wakati
wa Kikao cha
Tathimini cha Maadhimisho
ya siku 16 za kupinga ukatili wa kijinsia kilichoandaliwa na Vituo vya Taarifa
na Maarifa vinavyowezeshwa na Mtandao wa
Jinsia Tanzania TGNP.
Amesema
wazazi na walezi wanawajibu wa kuhakikisha watoto
wanapata huduma zote muhimu wanapokuwa
shuleni.
"Watoto
wetu tumekuwa tukiwakatili hawali chakula shuleni, tafisiri ya elimu bila
malipo inamaanisha hakuna kulipa ada na vile ambavyo tulikuwa tukilipia kama
wazazi, lakini mzazi unawajibu wa kumhudumia mtoto akiwa shuleni" Amesema
Mhe. Andason.
"Kwahiyo
niombe wazazi ni jukumu letu la msingi kuhakikisha yale mahitaji muhimu kwa
mtoto unashiriki kikamilifu ikiwemo chakula mashuleni" Amesema Mhe. Andason.
Kwa
upande wake Katibu wa Vituo vya Taarifa na Maarifa Wilaya ya Kishapu Bwana
Peter Nestory amesema wamefanikiwa
kuelimisha jamii juu ya ukatili wa kijinsia kupitia mikutano ya hadhara pamoja
na midahalo mbalimbali.
"Tumetoa
elimu kupitia mikutano ya hadhara, kuendesha midahalo, kutoa elimu ya kijinsia
shuleni kwa wanafunzi ambao wamekuwa wahanga wa vitendo vya ukatili na hivyo
kubaini kwamba Watoto wengi wamekuwa wakibakwa , kulawitiwa, kupata mimba za
utotoni na kusababisha watoto kupoteza ndoto zao na jamii kumaliza kesi
kindugu" Amesema Bwana Peter.
Kwa
upande wake Mratibu wa Vituo vya Taarifa na maarifa Bi.Fredina Saidi ameitaka jamii kuendelea kutoa taarifa za vitendo vya ukatili na
kuwafichua watu wanaofanya vitendo hivyo ili kujenga ustawi wa jamii na watoto
kufikia ndoto zao
"Niwaombe
mtoe taarifa ambazo zitasaidia kutokomeza ukatili lengo letu ni kuwa na jamii
salama. Pia hata watoto wafikie ndoto zao maana msipotoa na kufichua vitendo
vya ukatili vitaendelea kuleta athari katika jamii"Amesema Bi. Fredina.
Nae Afisa Maendeleo
ya Jamii Halmashauri ya Wilaya Ya Kishapu Bwana Joseph Swalala amewataka wadau wa kikao hicho kuwa mstari wa mbele
kusimamia maadhimio ya kikao ili kufikia
malengo ya kupinga na kutokomeza ukatili wa kijinsia katika jamii.
"Popote
tunapokuwa tuongelee ajenda ya ukatili, tumeadhimia watoto wapate chakula
shuleni kwahiyo tuhakikishe shule zinapofunguliwa watoto wanaanza kupata
chakula, wazazi na walezi kuwajibika katika suala la malezi hivyo tutaendeleza
kushirikiana kupinga ukatili" Amesema Bwana Swalala
Baadhi
ya wananchi waliohudhuria kikao hicho wameahidi kuwa mabalozi katika kuelimisha
jamii nyingine na kwamba wanaunga mkono maadhimio ya kikao ikiwemo suala la watoto
kupata chakula shuleni.
Disemba 10, 2022 Vituo vya taarifa na maarifa Wilaya ya Kishapu kwa kushirikiana na wadau
mbalimbali wa kupinga ukatili wa kijinsia wamefanya
kikao cha Tathimini ya kilele cha
maadhimisho ya siku 16 za kupinga ukatili wa
kijinsia.
Kaimu Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Kishapi Mhe.
Andason Mandia akitoa hotuba katika kikao cha Tathimini ya Maadhimisho ya siku
16 za kupinga ukatili
Mratibu wa vituo vya taarifa na maarifa wilaya ya
kishapu Bi. Fredina Saidi akizungumza
katibu wa vituo vya taarifa na maarifa wilaya ya kishapu Bwana peter Nestory akisoma taarifa ya utekelezaji
Afisa Maendeleo ya jamii wa Halmashauri ya wilaya ya Kishapu Bwana Joseph
Swalala akizungumza wakati wa kikao







Post a Comment