ASKOFU SANGU AWATAKA WAAMINI WAPYA KUYASHIKA MAFUNDISHO YA IMANI, PAROKIA YA LUBAGA- SHINYANGA
Misalaba0
Askofu wa Jimbo Katoliki Shinyanga Mhashamu Liberatus Sangu, amewapongeza Waamini wa Parokia ya Lubaga kwa moyo wao wa majitoleo, hatua ambayo imewezesha wanunue eneo lenye ukubwa wa Hekari 4 kwa ajili ya ujenzi wa Kigango cha Bushushu.
Akizungumza baada ya kufanya ziara ya kichungaji ya siku moja katika Parokia hiyo, amesema kupitia moyo wa majitoleo ambao wanaufanya Waamini wa Parorokia hiyo ya Lubaga, wanapata baraka nyingi kutoka kwa Mwenyezi Mungu na kujiwekea hazina mbinguni, baada ya maisha yao ya hapa duniani.
Amewasihi kuendelea kusali ili Mungu awawezeshe kuliendeleza eneo hilo, ambapo pamoja na kujenga Kanisa, pia waweze kujenga nyumba ya Watawa pamoja na huduma nyingine za kijamii, ikiwemo shule ya awali.
Askofu Sangu amebainisha kuwa, eneo hilo lina mchango mkubwa katika kusogeza huduma za kiroho kwa watu, na anatamani kuona siku moja Bushushu inakuwa Parokia mpya.
Aidha, Askofu Sangu amempongea Diwani wa Kata ya Lubaga Bw. REUBEN DOTTO, kutokana na juhudi alizozifanya katika kufanikisha kupatikana kwa eneo hilo, na amemtunuku hati maalum ya kutambua mchango wake kwa kanisa.
Wakati huohuo, amewataka Waamini wapya aliowapa Sakramenti ya Kipaimara kuyashika mafundisho yote ya imani waliyopewa, pamoja na kuishi kwa wema, upendo, amani na maadili mema.
Akiwa Katika Parokia hiyo ya Lubaga kwa ziara ya siku moja, ambayo imefanyika Jumapili tarehe 07.01.2023, Askofu Sangu ameweka jiwe la msingi na kubariki katika eneo ambako kutajengwa Kigango cha Bushushu, kuwaimarisha Wakristo wapya 103, kubariki ndoa 39 zilizodumu kwa miaka mitano na kuendelea pamoja na kupokea michango ya kulitegemeza Jimbo iliyochangwa na Waamini wa Parokia hiyo.
Askofu Sangu akipokelewa na Paroko wa Parokia ya Lubaga Padre James Misana katika Eneo la Bushushu ambako kutajengwa Kigango cha BushushuAskofu Sangu akiwa na mwenyeji wake (Padre James Misana) kuelekea katika eneo la kuweka jiwe la msingi kwa ajili ya ujenziAskofu Sangu akikata utepe katika eneo la ujenzi kabla ya kuweka jiwe la msingi, mwenye kanzu nyeusi ni Paroko msaidizi wa Parokia ya Lubaga Padre Paul Mahona na nyuma ya Askofu ni Katibu wa Askofu Padre Deusdedith KisumoAskofu Sangu akiweka jiwe la msingi katika eneo la mradiAskofu Sangu akiongoza sala maalum ya kubariki eneo la mradi wa ujezni wa kigango mara baada ya kuweka jiwe la msingiAskofu Sangu akibariki eneo kwa maji ya barakaAskofu sangu akifukiza ubani jiwe la msingiWaimarishwa wakimpokea Askofu Sangu katika Kanisa la Mt. Yohane Paul II makao makuu ya Parokia ya LubagaAskofu Sangu pamoja na Mapadre akiwa katika nyumba ya Mapadre Parokia ya Lubaga wakifurahia muda mfupi baada ya kuwabariki Waimarishwa waliompokeaParoko wa Parokia ya Lubaga Padre James Misana akimkaribisha Mhashamu Baba Askofu Sangu kwa ajili ya adhimisho la Misa na kuwatambulisha Waimarishwa pamoja na wanandoa waliobariki ndoa zao.Wanakwaya wa Parokia ya Lubaga wakiwa KanisaniParoko msaidizi wa Parokia ya Lubaga Padre Paul Mahona akisoma somo la InjiliAskofu Sangu akitoa mafundisho ya imani (Homilia)kwa Waaminiwa Parokia ya LubagaAskofu Sangu akitoa Sakramenti ya Kipaimarakwa WaimarishwaBaadhi ya Wanandoa wakijiandaa kurudia ahadi zao za ndoawanandoa wakiwa wameandaa pete zao kwa ajili ya kubarikiwa kabla ya kuvishanaAskofu Sangu akibariki peteWanandoa wakivishana peteWanandoa wakirudia ahadi zao za ndoa mbele ya Askofu Askofu Sangu akiwakabidhi wanandoa vyeti maalum na kuwapongezaAskofu Sangu akiwakomunisha Waimarishwa na Waamini wengineAskofu Sangu akiwa Kanisani katika adhimisho la Misa (katikati) ni Katibu wa Askofu Padre Deusdedith Kisumo na kulia ni Paroko msaidizi wa Parokia ya Lubaga Padre Paul MahonaBaadhi ya waamini wa Parokia ya Lubaga wakiwa KanisaniAskofu Sangu katika Picha ya pamoja na baadhi ya WaimarishwaAskofu Sangu akimtunuku cheti na kumpongeza Diwani wa Kata ya Lubaga Reuben Dotto kwa mchango wake katika utume wa KanisaMwenyeki wa Halmashauri walei Parokia ya Lubaga Bw. Willium Chami akitoa taarifa ya ParokiaAskofu Sangu akiwa na Paroko wa Parokia ya Lubaga (kushoto) Padre James Misana, Katibu wa Askofu Padre Deusdedith Kisumo (wa pili kulia ) na Paroko msaidizi wa Parokia ya Lubaga Padre Paul Mahona (wa kwanza kulia) wakifautaili Risala ya Parokia
Post a Comment