Na Mapuli Misalaba, Shinyanga
Jumuiya ya Umoja wa wanawake wa chama
cha mapinduzi CCM Wilaya ya Shinyanga mjini kesho itaadhimisha Miaka 46 ya
kuzaliwa kwa CCM kwa kufanya shughuli mbalimbali za kijamii ikiwemo kupanda miti.
Katibu wa UWT Wilaya ya Shinyanga mjini
Lucy Enock ameeleza kuwa shughuli hizo zitakwenda sanjari na mkutano wa hadhara
utakaofanyika kata ya Masekelo Manispaa ya Shinyanga.
Wakati akizungumza na Misalaba Blog katibu
huyo amesema pamoja na mambo mengine maadhimisho hayo yatahusisha zoezi la
usajiri wa kadi za wanachama wa jumuiya hiyo, kupanda miti katika taasisi mbalimbali
za serikali zilizopo katika kata hiyo pamoja na kutembelea baadhi ya vituo vya
kulelea watoto wenye uhitaji.
“Kwa
umoja wetu na mshikamano nawakaribisheni sana katika mkutano wa hadhara ili mje
msikie yale yote yaliyoandaliwa na chama ambayo yanafanywa na chama ili
kuendelea kukidumisha chama chetu”.amesema
Lucy Enock
Mgeni rasmi katika maadhimisho hayo
anatarajiwa kuwa mjumbe wa Halmashauri kuu ya CCM Taifa kutoka Mkoa wa
Shinyanga Ndugu Gasper Kileo.
Post a Comment