" MWENYEKITI WA SENETI MKOA WA SHINYANGA AANZA ZIARA YA KUTEMBELEA VYUO 17, AKABIDHI VIFAA VYA KAZI IKIWEMO KAUNTA BOOK NA MAFAILI

MWENYEKITI WA SENETI MKOA WA SHINYANGA AANZA ZIARA YA KUTEMBELEA VYUO 17, AKABIDHI VIFAA VYA KAZI IKIWEMO KAUNTA BOOK NA MAFAILI

Mwenyekiti wa Seneti Mkoa wa Shinyanga, Jackson Aloyce Mwizarubi, ameanza rasmi ziara ya kutembelea vyuo takribani 17 vilivyopo mkoani humo, ikiwa ni sehemu ya kuimarisha uongozi wa wanafunzi, kusikiliza changamoto zao pamoja na kuhamasisha matumizi bora ya fursa zinazotolewa na serikali.

Katika ziara hiyo, Mwizarubi ameambatana na Katibu wa Seneti Mkoa wa Shinyanga Bwana Lukomanga Jinyage Jiboli, Katibu Hamasa wa Seneti Sharon Callist Mathias pamoja na Mjumbe wa kamati ya uratibu Seneti Mkoa wa Shinyanga Mercy Saimon Shauri ambapo wameanza kwa kutembelea vyuo mbalimbali ikiwemo Hill Forest College na VETA Kishapu.

Akizungumza na wanachuo wa Hill Forest College, Mwizarubi amewataka vijana kuthamini na kutumia kikamilifu fursa wanazopewa na serikali, hususan katika kupata elimu na ujuzi unaowawezesha kujiajiri au kupata ajira.

“Tuna kila sababu ya kumshukuru Mheshimiwa Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kuendelea kuridhia na kuidhinisha bajeti zinazolenga kuwasaidia vijana. Niwaombe sana vijana wenzangu, hasa waliopata fursa hizi, kuzitumia vizuri. Pia tuendelee kuunga mkono juhudi za serikali ya awamu ya sita, na pale tunapokutana na changamoto, tuwasilishe kwa viongozi wanaohusika,” amesema Mwizarubi.

Baadhi ya wanachuo wa Hill Forest College wanaonufaika na ufadhili wa serikali wameishukuru serikali kwa kuwapatia fursa ya kusoma bure, huku wakimpongeza Mwenyekiti wa Seneti kwa kuanzisha ziara hiyo ambayo wamesema ina umuhimu mkubwa kwa maendeleo yao na wameomba iwe endelevu.

Aidha, katika ziara hiyo, viongozi hao wametembelea pia Chuo cha VETA Kishapu, ambapo Mwizarubi amezungumzia mipango mbalimbali ya Seneti ikiwemo kuandaliwa kwa semina kubwa itakayowakutanisha wanachuo wote wa vyuo vya Mkoa wa Shinyanga ili kujadili fursa na changamoto zinazowakabili vijana.

Ameongeza kuwa Seneti ya Mkoa pia inatarajia kuratibu mahafali ya pamoja kwa wahitimu wa vyuo mbalimbali, hatua ambayo inalenga kuimarisha mshikamano na kutoa heshima kwa wanafunzi wanaohitimu masomo yao.

Katika hatua nyingine, Mwenyekiti huyo amesimamia uchaguzi wa viongozi wapya wa Seneti katika baadhi ya vyuo vilivyotembelewa, ambapo nafasi mbalimbali zikiwemo za mwenyekiti, katibu na viongozi wengine zimejazwa. Pia amekabidhi vifaa vya kazi kwa viongozi hao, ikiwemo vitabu vya kumbukumbu (counter books) na mafaili kwa ajili ya kuhifadhi taarifa za Seneti katika kila chuo.

Kwa upande wao, baadhi ya wanafunzi wa VETA Kishapu wamempongeza Mwizarubi kwa ziara hiyo, wakisema imeleta hamasa mpya kwa wanafunzi, huku wakieleza kuwa utoaji wa zawadi na vifaa ni jambo jipya ambalo halijawahi kufanywa tangu kuanzishwa kwa Seneti, na wameahidi kutoa ushirikiano wa karibu kwa viongozi hao.

Leo, ziara hiyo imefanikiwa kutembelea vyuo viwili, huku ikitarajiwa kuendelea katika vyuo vingine vya Mkoa wa Shinyanga katika siku zijazo.

Viongozi wa Seneti Mkoa wa Shinyanga wakiongozwa na Mwenyekiti Jackson Aloyce Mwizarubi wakiwasili VETA Kishapu, ikiwa ni sehemu ya ziara ya kutembelea vyuo 17 mkoani humo.


 SHY TALENT FILMS - CONTENT YA MWISHO DRAMA

 
🥃🍶 TUMIA VINYWAJI BORA VYA KAMPUNI YA EAST AFRICAN SPIRITS – BEI RAFIKI, LADHA SAFI BILA HARUFU MBAYA

  • Wasiliana nasi:
    📍 East African Spirits (T) Ltd
    📞 +255 767 650 806 | +255 652 096 254

Post a Comment

Previous Post Next Post