" WATUMISHI WA MAHAKAMA KANDA YA SHINYANGA WAKUMBUSHWA KUFANYA KAZI KWA WELEDI, WIKI YA KISHERIA YAANZA RASMI

WATUMISHI WA MAHAKAMA KANDA YA SHINYANGA WAKUMBUSHWA KUFANYA KAZI KWA WELEDI, WIKI YA KISHERIA YAANZA RASMI

Na Mapuli Misalaba, Shinyanga

Mkuu wa Wilaya ya Kishapu Joseph Mkude amewashauri watumishi wa Mahakama kuu ya Tanzania kanda ya Shinyanga kufanya kazi kwa weledi ikiwa ni pamoja na kufuata sheria, kanuni na miongozo mbalimbali ya utumishi wa umma.

Akizungumza kwa niamba ya mkuu wa Mkoa wa Shinyanga kwenye uzinduzi wa wiki ya kisheria yanayofanyika kwenye uwanja wa Zimamoto Nguzonane mjini Shinyanga.

DC Mkude pamoja na mambo mengine ametumia nafasi hiyo kuwaomba wananchi na wadau mbalimbali kujitokeza ili kunufaika na fursa hiyo huku akiwasisitiza watumishi wa Mahakama kuzingatia maadili ya utumishi wa umma na kwamba wananchi waweze kupata haki zao.

“Nawaomba wananchi ambao hawajabahatika kufika kwenye viwanja hivi kwa leo kujitokeza ama kushirikia kikamilifu katika wiki hii ya sheria kwani maonsho na utoaji elimu juu ya maswala mbalimbali ya kisheria yataendeleo kutolewa hadi tarehe moja  mwezi wa pili  2023 pia napenda kuwahimiza wananchi kuitumia mahakama katika kutafuta haki zao kwani ndicho chombo pekee chenye mamlaka ya mwisho katika utoaji wa haki Nchini”.

“Napenda kutoa wito kwa watumishi wa Mahakama kufanya kazi kwa weledi kwa kuzingatia maadili ya utumishi wa umma sheria, kanuni na miongozo mbalimbali ya utumishi wa umma”.amesema DC Mkude

Kwa upande wake Jaji Mfawidhi wa Mahakama kuu ya Tanzania kanda ya Shinyanga Athumani Matuma amesema lengo la maadhimisho hayo ni kutoa elimu kwa wananchi juu ya shughuli mbalimbali zinazotolewa na Mahakama.

“Malengo ya maadhimisho haya ni kutoa elimu kwa upana kwa wananchi juu ya shughuli mbalimbali zinazotolewa na Mahakama na maboresho yanayoendelea kufanyika ndani ya Mahakama lakini vile vile tunaendelea tunakuwa tunawashirikisha wadau wetu wa Mahakama ambao nao wanapata fursa ya kutoa elimu na mara nyingi shughuli hizo ambazo wanazitoa wakati mwingine zinapelekea uwepo wa migogoro na mashauri Mahakamani  kwahiyo tukitumia fursa hii ya wiki ya kisheria kwa kupata elimu sahihi kunauwezekano mkubwa tukaziepuka migogoro mingi”.amesema Matuma

Leo umapili Januari 22, 2023, Mahakama kuu ya Tanzania kanda ya Shinyanga kwa kushirikiana na wadau wengine wa Sheria, imezindua maadhimisho ya wiki ya sheria nchini, katika uwanja wa Zimamoto ambako elimu kuhusu masuala mbalimbali ya kisheria itaendelea kutolewa mpaka siku ya kilele tarehe Februari 1, Mwaka huu 2023.

Hafla hiyo pia imehudhuriwa na wadau, wananchi pamoja na viongozi mbalimbali wa serikali akiwemo Mkurugenzi wa Manispaa ya Shinyanga Jomaary Satura na Mstahiki Meya wa Manispaa ya Shinyanga Mh: Elias Ramadhan Masumbuko.

Kaulimbiu ya maadhimisho ya wiki ya sheria kwa mwaka huu inasema kuwa “utatuzi wa migogoro katika usuluhishi kwa ajili ya kukuza uchumi endelevu”

Mkuu wa Wilaya ya Kishapu Joseph Mkude akizungumza kwa niamba ya mkuu wa Mkoa wa Shinyanga kwenye uzinduzi wa wiki ya kisheria yanayofanyika kwenye uwanja wa Zimamoto Nguzonane mjini Shinyanga.

Jaji Mfawidhi wa Mahakama kuu ya Tanzania kanda ya Shinyanga Athumani Matuma akizungumza kwenye uzinduzi wa wiki ya kisheria yanayofanyika katika uwanja wa zimamoto Nguzonane mjini Shinyanga.

TAZAMA PICHA ZOTE HAPA CHINI 




Post a Comment

Previous Post Next Post