
Wazazi na walezi Mkoani Shinyanga wametakiwa kutumia raslimali walizo nazo kuwekeza kwenye elimu ya Watoto ili kuwapa urithi na kuwajengea Msingi thabiti wa kukabiliana na mazingira ya sasa yanayohitaji vijana wasomi.
Kauli hiyo imetolewa na Afisa elimu ya watu wazima Mkoa wa Shinyanga Dedan Rutazika kwa niaba ya afisa Elimu Mkoa, kwenye Jubilee ya Miaka kumi tangu kuanzishwa kwa shule ya awali na Msingi ya OLA iliyopo Lohumbo kata ya Didia Halmashauri ya Wilaya ya Shinyanga.
Amesema wazazi na walezi wanapaswa kuwekeza kwenye elimu ya Watoto kama msingi wa kuwaandaa kukabiliana na mazingira ya dunia ya sasa inayohitaji wasomi zaidi.
Afisa Elimu Rutazika amekumbusha Walimu pamoja na mafunzo mbalimbali wanayoendelea kuwapatia Wanafunzi lakini pia wanatakiwa kuwafundisha elimu ya kujitegemea ili kuwajengea uwezo wa kujitegea
Kwa upande wake sister Lita Dung ambaye ni Mwalimu mtangulizi katika shule ya OLA English Medium amesema mafanikio mbalimbali yaliyofikiwa shuleni hapo yamechangiwa na juhudi za Walimu na ushirikiano mzuri wa wazazi na walezi
Kwa upande wake Makamu wa Askofu jimbo katoliki la Shinyanga, Padri kizito Nyanga amepongeza juhudi za shirika la OLA kuwekeza miradi ya Elimu na afya katika Jimbo hilo,huku akiahidi ushirikiano Zaidi kwa taasisi hiyo ya dini.
Maadhimisho hao ya jubilee ya miaka 10 toka kuanzishwa kwa shule ya awali na msingi ya OLA yamefanyika katika shule hiyo iliyopo katika kata ya Didia Halmashauri ya Wilaya ya Shinyanga,ambayo ilitanguliwa na adhimisho la misa takatifu.



Afisa elimu ya watu wazima Mkoa wa Shinyanga Dedan Rutazika
Post a Comment