Kamati
ya kudumu ya Bunge ya Utawala na Serikali za Mitaa (USEMI) imeridhishwa na
utekelezaji unaoendelea wa miradi mbalimbali ya maendeleo katika Halmashauri ya
Manispaa ya Shinyanga kwa kutumia fedha za mapato ya ndani kwa lengo la kutatua
changamoto za wananchi.
Kamati
hiyo leo imetembelea na kukagua miradi mbalimbali ikiwemo ujenzi wa soko kuu la
kisasa la Mkoa wa Shinyanga pamoja na shule ya wasichana Butengwa iliyopo kata
ya Ndembezi ambapo Mwenyekiti wa kamati hiyo Mhe. Daniel Londo amepongeza
uongozi wa Halmashauri hiyo kwa matumizi sahihi ya fedha za mapato ya ndani.
Mhe.
Longo amesema Halmashauri hiyo imefanya ubunifu ambao utakuwa chachu kwa
maendeleo ya wananchi na Taifa kwa ujumla na kwamba ameziomba Halmashauri
zingine Nchini kuiga mfano kutoka katika Manispaa hiyo.
“Nipongeze sana watumishi wa
Halmashauri ya Manispaa ya Shinyanga kwa uzalendo mkubwa, weledi lakini kutanguliza
mbele maslahi makubwa ya Taifa tunapenda mtumike kama rejea kwa watumishi
wengine Tanzania miradi hii ambayo mmeitekeleza katika Halmashauri hii ya
Manispaa ya Shinyanga kama ingetekelezwa katika kila Manispaa ya Nchi hii
naamini kabisa safari yetu kuelekea kwenye mafanikio ingekuwa fupi na muda mchache
zaidi kuliko tunaoenda nao”
“Nikupongeze Mkurugenzi wa Manispaa
ya Shinyanga na timu yao uzalendo ambao unauonesha kamati imeuona rai yetu
tunaomba sana uendelee kuwa mzalendo kwa Nchi yao”amesema
Mhe. Longo
“Lakini kitendo cha wafanyabishara
kuukubali mradi wa soko kamati hii inauzoefu wa kupokea malalamiko katika
miradi ambayo inawahusisha wamachinga, wauzamitumba na wafanyabishara ndogo
ndogo katika safari zetu tumekuwa tukipokea malalamiko lakini hali hiyo imekuwa
tofauti sana kwa hapa Halmashauri ya Manispaa ya Shinyanga kwakweli
tunawapongeza sana”.amesema Mhe. Longo
Kwa
upande wake Naibu waziri ofisi ya Rais Tamisemi Deo Ndejembi wakati kamati hiyo
ikitembelea na kukagua ujenzi wa soko kuu la kisasa la Mkoa wa Shinyanga,
amesema Manispaa hiyo imefanya utekelezaji wenye tija ambao utawanufaisha
wafanyabishara wakubwa kwa wadogo.
“Naipongeza Halmashauri ya Manispaa
ya Shinyanga kwa kuja na mradi huu wa ubunifu lakini mradi ambao unatatua pia
kero za wafanyabiashara wadogo wadogo lakini pia Halmashauri hii kwa kutenga
fedha wamefanya jambo kubwa sana na nijambo la kuigwa na Halmashauri zingine
ambazo kwenye mapato ya ndani zinauwezo wa kutekeleza miradi mikubwa kama hii”.amesema
Naibu Waziri Ndejembi
Awali
akizungumza Mkurugenzi wa Manispaa ya Shinyanga Dkt. Jomaary Satura amesema
ujenzi wa soko kuu la kisasa la Mkoa wa Shinyanga unatekelezwa kwa kutumia
fedha za mapato ya ndani ambao utagharimu kiasi cha shilingi Bilion 1.8.
Mkurugenzi
Dkt. Satura amesema ujenzi wa soko kuu la kisasa la Mkoa wa Shinyanga ghorofa
moja itakuwa na vyumba 106 na kwamba mradi huo utawanufaisha wafanyabishara,
wananchi pamoja na Halmashauri katika ukusanyaji wa mapato ya ndani.
Baadhi
ya wabunge akiwemo mbunge wa viti maalum Mkoa wa Shinyanga kupitia chama
cha Demokrasia na Maendeleo CHADEMA Mheshimiwa Salome Makamba wameipongeza
Halmashauri kwa ubunifu huo wa miradi ya maendeleo ambayo itawanufaisha wananchi hasa wa Manispaa ya
Shinyanga.
Wabunge
hao pia wamesisitiza kuharakishwa kwa miradi hiyo ambapo wamesema endapo miradi
itakamilika kwa wakati itamaliza kero za wananchi ambao wengi wanatarajia
kunufaika.
Post a Comment