" KAMATI YA KUDUMU YA BUNGE YA UTAWALA, KATIBA NA SHERIA YAFANYA ZIARA SHINYANGA, YASISITIZA SERIKALI KUENDELEZA NA KUBORESHA MIRADI INAYOANZISHWA NA WANANCHI

KAMATI YA KUDUMU YA BUNGE YA UTAWALA, KATIBA NA SHERIA YAFANYA ZIARA SHINYANGA, YASISITIZA SERIKALI KUENDELEZA NA KUBORESHA MIRADI INAYOANZISHWA NA WANANCHI

Na Mapuli Misalaba, Shinyanga

Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Utawala, Katiba na Sheria imeikumbusha serikali kupitia Halmashauri zake  kuhakikisha inaendeleza miradi yote inayoanzishwa  na wananchi ili kuleta tija zaidi katika jamii.

Akizungumza baada ya kamati hiyo kutembelea na kukagua miradi mbalimbali ya maendeleo katika Manispaa ya Shinyanga, Makamu Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Utawala, Katiba na Sheria (Mb)Florent Kyombo amesema ni muhimu miradi inayoanzishwa na wananchi kuendelezwa ili kuleta matokeo chanya kwa uharaka.

Mhe. Kyombo amesisitiza kuwa serikali kupitia Halmashauri zake ni vyema kujenga tamaduni za kuendeleza na kuboresha miradi inayoanzishwa na wananchi  ili iweze kuleta manufaa Zaidi ikiwemo miradi inayotekelezwa na walengwa wa kaya maskini kupitia  mfuko wa maendeleo ya jamii TASAF.

---INSERTS…KYOMBO---

Makamu Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Utawala, Katiba na Sheria (Mb)Florent Kyombo amewaomba wananchi wa Mkoa wa Shinyanga kuendelea kushirikiana na serikali katika utekelezaji wa miradi ya maendeleo ili kufikia malengo yaliyokusudiwa.

Kwa upande wao baadhi ya wajumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Utawala, Katiba na Sheria akiwemo Mbunge wa jimbo la Kishapu Mhe. Boniphace Butondo wamewaasa wanufaika wa miradi ya TASAF kutumia vizuri fedha wanazopata katika utekelezaji wa miradi hiyo na kwamba waepuke matumizi mabaya ya fedha ikiwemo ulevi na mambo mengine yasiyofaa kwenye familia na jamii kwa ujumla.

Wajumbe wa kamati hiyo pia wameiomba serikali kushughulikia changamoto zinazowakabili walengwa wa kaya maskini ikiwemo changamoto ya upatikanaji wa namba za NIDA ambayo ni changamoto kubwa katika jamii.

Akizungumza Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Menejimenti ya utumishi wa Umma na  Utawala Bora, Mhe. Jenista Mhagama amesema katika utekelezaji wa miradi ya TASAF serikali imetenga fedha kiasi cha shilingi Bilioni 496 ambapo Bilioni 51.014 zitawanufaisha wakazi wa Mkoa wa Shinyanga.

Waziri Mhe. Mhagama amewasisitiza viongozi wa Halmashauri wanaosimamia fedha hizo kuhakikisha zinatumia vizuri ili kufikia malengo yaliyokusudiwa na serikali.

Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Bi Christine Mndeme amemshukuru Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kuleta fedha za utekelezaji wa miradi mbalimbali ya maendeleo ikiwemo sekta ya elimu, afya, pamoja na miundombinu.

Amesema Mkoa wa Shinyanga wananchi 44,252 wanaendelea kunufaika na mpango wa TASAF ambapo jumla ya miradi 598 inayosimamiwa na mpango wa TASAF Mkoa wa Shinyanga inaendelea vizuri.

RC Mndeme ameihakikishia Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Utawala na Katiba na Sheria kuwa Mkoa wa Shinyanga utaendelea kuibua na kuiendeleza miradi mbalimbali ya maendeleo kwa kushirikiana na jamii husika.

Aidha Mndeme amesema ataendelea kusimamia matumizi sahihi ya fedha za miradi mbalimbali ya maendeleo ili kuwasaidia wananchi kuinuka kiuchumi katika maisha yao ya kila siku.

Naye Mstahiki Meya wa Manispaa ya Shinyanga Mhe. Elias Radhaman Masumbuko amemshukuru Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kuleta fedha za maendeleo katika Manispaa hiyo ambapo ameahidi kuendelea kushughulikia changamoto zinazowakabili wananchi ili kuendana na kasi ya mabadiliko ya kimaendeleo.

Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Utawala, Katiba na Sheria pamoja na mambo mengine imetembelea na kukaguzi ujenzi wa jengo la Ofisi ya Taifa ya Mashtaka Mkoa wa Shinyanga ambalo linaendelea kujengwa kwa lengo la kusogeza karibu huduma za kimashtaka karibu na wananchi.

Akitoa taarifa za ujenzi wa jengo hilo kwa kamati hiyo, Naibu Waziri wa Katiba na Sheria Pauline Gekul amesema kuwa septemba 26 mwaka 2022 Ofisi ya Taifa ya Mashtaka iliingia Mkataba na Mkandarasi Eliroi Construction kwa ajili ya ujenzi wa jengo la Ofisi ya Mashtaka Mkoa wa Shinyanga wenye thamani ya Bilioni 2.15 ikijumuisha ongezeko la Thamani VAT.

Gekul amesema kuwa mradi huo una Taraji kukamilika ndani ya muda wa miezi 8 ambapo ulianza kuteklelezwa November 22,2022 ambapo unataraji kukamilika June 22 ambapo mpaka sasa umefikia asilimia 35.

Bi Gekul ameongeza kwa kusema kuwa mpaka sasa mkandarasi amekwisha lipwa fedha za awali kiasi cha shilingi milioni 323 kati ya bilioni 2.15 huku Mkandarasi Mshauri Mwelekezi wa mradi Water Institute kawazulite maombi ya kulipwa kiasi cha shilingi milioni 335.5 

Kwa upande wake Mkurugenzi wa Mashtaka (DPP) Sylvester Mwakitalu ameishukuru Kamati hiyo kwa juhudi zake kubwa za kuipigania Ofisi hiyo ambapo kwa mwaka huu wa fedha unaondelea jumla ya mikoa sita imepatiwa fedha za ujenzi wa Ofisi ikiwa ni pamoja na Shinyanga,Geita,Manyara, Rukwa, Katavi na Njombe na kufanya idadi ya ofisi zinazojengwa kufikia kumi.

DPP Mwakitalu ameushukuru uongozi wa Mkoa wa Shinyanga chini ya Mkuu wa Mkoa huo Christine Mndeme kwa kuwapatia eneo la Kiwanja kwa ajili ya ujenzi wa Ofisi hiyo ambayo itasaidia na kurahisisha utoaji wa huduma kwa jamii juu ya masuala ya Mashtaka ambapo amesema eneo hilo awali ilipewa taasisi nyingine.

DPP Mwakitalu amesema kuwa ujenzi huo utakapokamilika utarahisisha utaoaji wa huduma kwa jamii ambapo watumishi watakuwa na sehemu bora na mazingira rafiki ya utaoji wa huduma kwa wananchi.

Mkandarasi anayetekeleza ujenzi wa mradi huo kampuni ya Eliroi Construction Bw Ngakuka Ngakuka amesema kuwa mradi huo umechelewa kufikia asilimia 50 mpaka sasa kutokana na kuchelewa kwa malipo ya awali sambamba hilo Ngakuka amesema kuwa licha ya kuraisi cheti cha malipo yanakwama kutoka kwa wakati 

Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Utawala na Katiba na Sheria imefanya ziara ya kukagua na kutembelea miradi mbalimbali inayotekelezwa na Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania katika Manispaa ya Shinyanga.





Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Bi Christine Mndeme akizungumza







Mtahiki Meya wa Manispaa ya Shinyanga Elias Ramadhan Masumbuko akimshukuru Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan.











Post a Comment

Previous Post Next Post