Suzy Luhende, Misalaba Blog
Kamati ya kusimamia usambazaji wa viuatilifu na vinyunyizi Tanzania imefanya ufuatiliaji katika mikoa 17 inayolima zao la pamba
na kubaini baadhi ya viongozi wa vyama vya msingi(AMCOS) kujihusisha na vitendo vya wizi wa viuatilifu na vinyunyizi na wengine kughushi taarifa za fomu za viuadudu ambapo tayari kesi sita za viongozi hao zimefikishwa mahakamani.
Akitoa taarifa ya utekelezaji wa kamati hiyo kwa vyombo vya habari mjini Shinyanga mwenyekiti msaidizi wa kamati ya usambazaji wa viuadudu na vinyunyizi Protas Henry leo amesema lengo la kamati hiyo ni kusimamia usambazaji wa viuadudu vya zao la pamba na vinyunyizi kuanzia katika maghala ya bodi hadi vinapowafikia wakulima na kuhakikisha viuadudu na vinyunyizi vinawafikia kwenye maghala ya bodi ya pamba.
Henry amesema baada ya kuzunguka mikoa yote wamebaini changamoto hizo zikiwemo za baadhi ya AMCOS kughushi taarifa za kwenye fomu ya kugawia viuadudu, na kutojazwa fomu kwa usahihi na kwa makusudi kwa nia ya kutengeneza mianya ya rushwa ya wizi wa pembejeo husika, pia kuna baadhi ya viongozi wa AMCOS kutozingatia utaratibu wa ugawaji wa viuadudu na vinyunyizi, ambapo kufanya hivyo haitakiwi ni kosa la kisheria.
Aidha amesema kamati hiyo imeendelea kutekeleza majukumu yake tangu mwezi Desemba 2022 hadi sasa, ambapo imekwishafanya ukaguzi wa mara kwa mara kwenye AMCOS ambazo zinahusika moja kwa moja na ugawaji wa viuadudu na vinyunyizi katika wilaya ya Tanganyika, Mpanda, Nyang'wale, Chato, Geita, Bariadi, Kishapu, Maswa, Kwimba, Misungwi, Busega, Bunda, Itilima, Meatu, Igunga, Sengerema, Kahama,na kazi hiyo inaendelea.
Pia amesema wizara imeweka mazingira wezeshi yatakayoongeza uzalishaji wa pamba kutoka tani 174,032 katika msimu wa 2021/2022 hadi tani 500,000 msimu 2022/2023, ili kufanikisha lengo hilo bodi ya pamba Tanzania imeweka malengo ya kununua na kusambaza ekapaki za viuadudu 9,800,000, vinyunyizi 37,400 wamenunuliwa.
"Bakaa ya msimu uliopita ni ekapaki 3,500,000 na vinyunyizi 11,000, hivyo hadi sasa takriban ekapaki 8,303,160 na vinyunyizi 42,584 vimeshasambazwa kwa wakukima wa zao la pamba katika maeneo yote yanayozalisha zao hilo"amesema Henry.
"Ili kuwa na matokeo chanya katika kipindi hiki cha Rais Samia Suluhu kuna mikakati ya kuongeza zao la pamba ambapo waziri wa kilimo Hussein Bashe aliagiza kuunda kamati ya kudimamia usambazaji wa viuadudu na vinyunyizi vya zao la pamba kuanzia kwenye maghala hadi kwa wakulima ambapo kamati hiyo inaundwa na jumla ya watu 10 ambao ni maafisa wa serikali kutoka mamlaka ya usimamizi wa afya ya mimiea na Viuatilifu Tanzania (TPHPA)"ameongeza.
Kwa upande wake Kaimu mkurugenzi mkuu wa bodi ya pamba Tanzania James Shimbe amesema Bodi ya pamba imejipanga vizuri kuhakikisha inamuunga mkono Rais Samia Suluhu kwa kuwajali wakulima, ambapo msimu wa 2022/2023 wamesambaza mbegu za pamba tani 22, 000 zenye thamani ya zaidi ya Sh 1 bilioni na waliagixa viuadudu zaidi ya milioni 11 zenye thamani ya Sh 51 bilioni.
"Lengo kubwa kuwasambazia wakulima ili kukabiliana na wadudu na kwa kufikia tarehe ya leo viuawadudu milioni 8 yenye thamani ya Sh 35 bilioni na tunategemea kupata mavuno zaidi ya tani laki 4 za pamba na tunatarajia kupata kilo milioni 400 kutakuwa na ongezeko kwa sababu hali ya hewa ni nzuri, na vinyunyizi vimesambazwa kwa wakulima wa zao la pba katika maeneo yote yanayozalisha zao hilo, ns hadi sasa wamenunua ndege 20 kwa ajili ya kunyunyuzia mashamba makubwa"amesema Shimbe.
Pia amewataka wananchi wazingatie wakati wa kunyunyizia pamba ambapo wanatakiwa kunyunyizia asubuhi wakiwa wadudu wamejitokeza, lakini wakinyu yizia mchana wadudu hao hawafi wanakuwa wamejificha, hivyo unaweza kunyunyuzia lakini ukabaki na malalamiko kwamba dawa hiyo ni feki kumbe hukuzingatia muda.
Naye afisa kilimo mwanadamizi bodi ya pamba Tanzania Renatus Luneja amesema TCB inataka pembejeo zilindwe na ziwafikie walengwa huku akowatakawakulima kufikakatika AMCOS kwa ajili ya kuchukuapembejeo zakilimo
Kaimu mkurugenzi mkuu wa bodi ya pamba Tanzania James Shimbe akizungumza juu ya viuatilifu.

Post a Comment