Na Mapuli Misalaba, Shinyanga
Wito umetolewa kwa
waislam wote Wilaya ya Shinyanga kuishi matendo yanayompendeza Mwenyezi Mungu
hasa katika kipindi hiki cha Mwezi Mtukufu wa Ramadhan.
Wito huo umetolewa leo na
Shekhe wa Wilaya ya Shinyanga Sudi Kategile wakati akizungumza na Misalaba Blog
ilipomtembelea ofisini kwake.
Kategile amewataka waislam
kutumia kipindi hiki cha Mwezi Mtukufu wa Ramadhan kutenda matendo mema bila
kubagua Dini wala kabila
Ametumia fursa hiyo
kuwasisitiza waislam wote kutekeleza ibada ya funga katika kipindi hiki cha Mwezi
mtukufu wa Ramadhan.
Wakati huo huo Shekhe
Kategile amewakumbusha waamini wa dini ya kiislam kuendelea kuomba Amani ya
nchi ikiwa ni pamoja na kuombea viongozi wa serikali
Leo Waislam wameingia
katika mwezi huu mtukufu wa Ramadhan kwa siku 30, ndani ya wiki nne zijazo
ambapo mamilioni ya waislamu watajinyima
kula na kunywa kuanzia mapema alfajiri hadi jioni.
Post a Comment