Na Mapuli Misalaba, Shinyanga
Mkurugenzi wa Taasisi ya waandishi wa habari mtandaoni (Tanzania Online Media Alliance) TOMA Seif Mangwangi leo amekutana na kuzungumza na baadhi ya waandishi wa habari za mtandaoni Mkoa wa Shinyanga.
Kikao hicho kimefanyika katika ukumbi wa Mazingira Center Mjini Shinyanga ambapo pamoja na mambo mengine Mkurugenzi Mangwangi ameelezea faida za waandishi wa habari hao kujiunga na Taasisi ta TOMA katika utekelezaji wa majukumu ya kila siku.
Bwana Seif Mangwangi ametumia nafasi hiyo pia kuelezea majukumu ya TOMA katika Tasnia ya habari huku akihamasisha waandishi hao kujiunga na taasisi ya waandishi wa habari mtandaoni (TOMA) ambayo inapokea waandishi wote wenye utayari hapa Nchini.
Taasisi ya waandishi wa habari mtandaoni (Tanzania Online Media Alliance) TOMA inasimamia vyombo mbalimbali vya habari ikiwemo Blogs na Online Tv katika mikoa mbalimbali Nchini Tanzania kwa kutatua kero na changamoto ikiwa ni pamoja na kutoa fursa mbalimbali kwa waandishi wa habari za mtandaoni.
Post a Comment