Na Mapuli Misalaba, Shinyanga
Mkuu wa Wilaya ya Shinyanga Mhe. Johari Samizi amesema
miradi mbalimbali ya maendeleo yenye jumla ya fedha zaidi ya Bilion 13 imetekelezwa
katika Halmashauri ya Manispaa ya Shinyanga
kwa kipindi cha mwezi Januari hadi Disemba 2022 ikiwa ni utekelezaji wa
ilani ya CCM.
Ameyasema hayo wakati akiwasilisha taarifa ya utekelezaji wa
ilani ya uchaguzi ya Chama cha Mapinduzi CCM ya Mwaka 2020 hadi 2025 kipindi
cha Julai hadi Disemba Mwaka 2022 kwenye mkutano ambao umefayika katika ukumbi
wa ofisi za CCM Wilaya ya Shinyanga mjini na kuhudhuriwa na viongozi mbalimbali
wa chama pamoja na viongozi wa serikali wakiwemo wakuu wa idara katika
Halmashauri ya Manispaa ya Shinyanga.
DC Samizi amesema pato la
wastani la mkazi wa Manispaa ya Shinyanga kwa Mwaka 2021 ni (zaidi ya Milioni
moja) shilingi 1,861,770 kwa Mwaka.
Amesema Halmashauri ya
Manispaa ya Shinyanga katika utekelezaji wa ilani ya CCM imetekeleza miradi
mbalimbali ya maendeleo kwenye sekta mbalimbali ikiwemo sekta za Elimu, Afya,
ujenzi na maendeleo ya jamii, barabara na maji na kwamba miradi hiyo ina
thamani ya jumla Tshs Bilioni 13,804966,547 katika Manispaa ya Shinyanga.
Mkuu wa Wilaya
ya Shinyanga Mhe. Johari Samizi amefafanua zaidi kuwa miradi hiyo ilihusisha
ujenzi wa mashule, maeneo ya kutolea huduma za afya kama kituo cha afya na
zahanati, majengo ya ofisi, kituo cha mabasi, mikopo kwa vikundi, barabara,
miundombinu ya maji pamoja na sekta zingine.
Ametaja baadhi ya kata za Manispaa ya Shinyanga
zilizofikiwa na miradi hiyo kuwa ni pamoja na kata ya Kambarage, Ngokolo,
Ndembezi, Old Shinyanga, Ndala na kata ya Chamaguha.
Amesema Serikali katika kipindi hicho ilitoa fedha kwa
ajili ya utekelezaji wa miradi mbalimbali ya maendeleo ambapo iliagiza kujenga
na kuimarisha vituo vya kutolea huduma za afya ili viweze kutoa huduma bora
zaidi kwa wananchi hadi kufikia Mwaka 2025 ambapo serikali itaongeza vituo vya
kutolea huduma za afya kwa asilimia 20 ya vituo.
Mhe. Samizi ameelezea zaidi maagizo mengine ya
serikali kuwa ni pamoja na kuwezesha
vijana kushiriki katika shughuli za ujasiriamali ikiwemo kuwapa mafunzo na
kuwaunganisha na kuwawezesha mikopo ya fedha kwa vikundi, ukarabati wa
miundombinu ya elimu pamoja na kuhifadhi na kuendeleza mazingira ya shule
ikiwemo shule mpya ya mtaa wa Azimio katika kata ya Lubaga, ujenzi wa choo
sekondari Kizumbi, ujenzi wa miundombinu shule ya wasichana Butengwa kata ya
Ndembezi.
Amesema maagizo mengine ya serikali ni kuongeza ajira,
kuboresha kasi ya utekelezaji awamu ya tatu ya TASAF ili kuwafikia wananchi
maskini katika vijiji, mitaa yote kwa kutekeleza miradi ya kutoa ajira za muda
ili kukuza uchumi wa kaya na kuendeleza rasilimali watu lakini pia amesema pamoja na kuongeza upatikanaji wa huduma ya
maji na usafi wa mazingira vijiji kutoka asilimia 63 hadi asilimia 85 ifikapo
Mwaka 2025.
Aidha Mkuu wa Wilaya ya Shinyanga Mhe. Johari Samizi
katika taarifa yake ameelezea shughuli mbalimbali zinazoendelea kufanyika
katika Manispaa ya Shinyanga.
“Manispaa
ya Shinyanga ni miongoni mwa Halmashauri mbili zinazounda Wilaya ya Shinyanga Halmashauri
hii inapakana na Halmashauri ya Wilaya ya Shinyanga upande wa Kaskazini
Magharibi na Kusini Magharibi, na Kishapu kwa upande wa Mashariki na Kusini
Mashariki”.
“Manispaa
ina eneo la kilometa za mraba 548 ambapo kati ya eneo hilo, eneo la katikati ya
mji lina kilometa za mraba 25 na eneo mchanganyiko na vijiji ni kilometa za
mraba 523 shughuli kuu za kiuchumi ni kilimo na ufugaji, viwanda na Biashara na
shughuli za maofisini”.amesema DC Samizi
“Kwa
mujibu wa Sensa ya watu na makazi iliyofanyika Nchi nzima Mwaka 2012
Halmashauri ya Manispaa ya Shinyanga ilikuwa na jumla ya watu 161,391 ambapo
kwa sasa kwa mujibu wa mamlaka ya takwimu Tanzania (NBS) kwa Mwaka 2020
Manispaa inakadiriwa kuwa na idadi ya watu wapatao 201,797 ambapo wanaume ni
98,289 na wanawake ni 103,508”.
“Kiutawala
Halmashauri ya Manispaa ya Shinyanga ina tarafa tatu (3) kata kumi na saba
(17), vijiji kumi na saba (17) mitaa 55 na vitongoji 84 katika kila ngazi kuna
watendaji na viongozi thabiti waliochaguliwa na wananchi”.amesema
DC Samizi
“Hali
ya usalama ni shwari ukiacha matukio ya hapo na pale yanayoripotiwa na jeshi la
polisi Manispaa imekuwa ikijitahidi kuwa mstari wa mbele katika kupiga vita vitendo
vyote vya ukatili, ubaguzi na unyanyapaa kwa makundi yote”.
“Shughuli
kuu za kiuchumi kwa Manispaa ya Shinyanga ni kilimo, ufugaji, biashara ajira za
maofisini na shughuli za viwandani, asilimia 70 ya wakazi wa Halmashauri ya
Manispaa ya Shinyanga hujishughulisha na kilimo na ufugaji mazao makuu ya
chakula ni mahindi, mpunga, mtama, uwele, muhogo, viazi vitamu, dengu, choroko
na karanga mazao ya biashara ni Pamba na Alizeti”.amesema
DC Samizi
Wajumbe wa Halmashauri
kuu ya CCM Wilaya ya Shinyanga mjini wameipokea taarifa ya utekelezaji wa ilani
ya chama cha mapinduzi CCM ya Mwaka 2022/2023 katika kipindi cha Julai hadi
Disemba Mwaka 2022.
Katika mkutano huo
wajumbe wa Halmashauri kuu ya CCM Wilaya ya Shinyanga mjini wameipongeza
serikali kwa kuendelea kutekeleza ilani ya chama hicho huku wakimshukuru Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan.
Aidha wajumbe wa mkutano
huo wamepata nafasi ya kutoa ushauri, maoni na kuuliza maswali mbalimbali juu
ya changamoto zinazowakabili wananchi ambapo wataalam kutoa Halmashauri ya
Manispaa ya Shinyanga wamejibu maswali hayo huku Mkuu wa Wilaya ya Shinyanga
Mhe. Johari Samizi akipokea na kuahidi kwenda kushughulikia kero za wananchi.
Mkuu wa Wilaya ya Shinyanga Mhe. Johari Mussa Samizi akisoma taarifa ya utekelezaji wa ilani ya uchaguzi ya Chama cha Mapinduzi CCM ya Mwaka 2020 hadi 2025 kipindi cha Julai hadi Disemba Mwaka 2022 mbele ya wajumbe wa Halmashauri kuu ya CCM Wilaya ya Shinyanga mjini.

Mwenyekiti
wa CCM Wilaya ya Shinyanga Mhe. Anord Makombe akizungumza kwenye mkutano huo wa
Halmashauri kuu ya CCM Wilaya ya Shinyanga mjini.
Mwenyekiti
wa CCM Wilaya ya Shinyanga Mhe. Anord Makombe akizungumza kwenye mkutano huo wa
Halmashauri kuu ya CCM Wilaya ya Shinyanga mjini.
Katibu
wa CCM Wilaya ya Shinyanga Bwana Ally
Bin Ally akizungumza kwenye mkutano huo wa Halmashauri kuu ya CCM Wilaya ya
Shinyanga mjini.
Katibu
wa CCM Wilaya ya Shinyanga Bwana Ally
Bin Ally akizungumza kwenye mkutano huo wa Halmashauri kuu ya CCM Wilaya ya
Shinyanga mjini.
Mstahiki
Meya wa Manispaa ya Shinyanga Mhe. Elias Ramadhan Masumbuko akizungumza kwenye
mkutano huo wa Halmashauri kuu ya CCM Wilaya ya Shinyanga mjini.
Katibu
wa Mbunge jimbo la Shinyanga Bwana Samwel Thobias akitoa salam za Mbunge kwenye
mkutano huo.
Katibu wa itikadi, siasa na uenezi Wilaya ya Shinyanga mjini Bwana Said Bwanga akizungumza kwenye mkutano huo wa Halmashauri kuu ya CCM Wilaya ya Shinyanga mjini.
Wajumbe
wa Halmashauri kuu ya chama cha mapinduzi CCM Wilaya ya Shinyanga mjini wakiwa
katika mkutano huo wa kupokea taarifa ya utekelezaji wa ilani ya CCM kipindi cha
Julai hadi Disemba Mwaka 2022.

Wajumbe wa Halmashauri kuu ya chama cha mapinduzi CCM Wilaya ya Shinyanga mjini wakiwa katika mkutano huo wa kupokea taarifa ya utekelezaji wa ilani ya CCM kipindi cha Julai hadi Disemba Mwaka 2022.

Wajumbe wa Halmashauri kuu ya chama cha mapinduzi CCM Wilaya ya Shinyanga mjini wakiwa katika mkutano huo wa kupokea taarifa ya utekelezaji wa ilani ya CCM kipindi cha Julai hadi Disemba Mwaka 202
Mmoja wa wajumbe wa Halmashauri kuu ya CCM Wilaya ya Shinyanga mjini akiuliza swali kwenye mkutano huo.
Mmoja wa wajumbe wa Halmashauri kuu ya CCM Wilaya ya Shinyanga mjini akiuliza swali kwenye mkutano huo.Mmoja wa wajumbe wa Halmashauri kuu ya CCM Wilaya ya Shinyanga mjini akiuliza swali kwenye mkutano huo.
Mmoja wa wajumbe wa Halmashauri kuu ya CCM Wilaya ya Shinyanga mjini Mhe. Victor Mkwizu akitoa ushauri kwenye mkutano huo.
Mmoja wa wajumbe wa Halmashauri kuu ya CCM Wilaya ya Shinyanga mjini akiuliza swali kwenye mkutano huo.
Akizungumza kwa niaba ya Mkurugenzi wa Manispaa ya Shinyanga, Mkuu wa idara ya maendeleo ya jamii Halmashauri ya Manispaa ya Shinyanga Bwana John Tesha.
Post a Comment