Na: Belnardo Costantine, Misalaba Media
Jeshi la Polisi Nchini limethibitsha limetoa taarifa inayo eleza kumkamata Bi. Brenda Rupia Jonas mwanachama wa chama cha demekrasia na maendeleo "CHADEMA" mbaya pia ni Mkurugenzi wa Mawasiliano wa Chama hicho.
Kwa Mujibu wa Taarifa iliyotolewa na Msemaji wa Jeshi la Polisi nchini DCP. David Misime imeeleza kuwa Bi. Rupia amekamatwa kwa ajili ya mahojiano kutokana na tuhuma zinazomkabili ikiwemo kutoa taarifa za uongo na za uchochezi.
Hata hivyo taarifa imeleza kuwa baada ya mahojiano taratibu nyingine kwa mujibu wa sheria za nchi zitafuata.
Sambamba na hilo CHADEMA ilitoa taarifa ya kuzuiwa kwa Mkurugenzi huyo ambaye alikuwa safarini kuingia Nchini Kenya kwaajili ya kikao kilicho kilichopangwa kabla ya kwenda Munich Ujerumani Kushiriki mafunzo ya kuhusu Demokrasia na Uchaguzi.
Post a Comment