Na Mapuli Misalaba, Shinyanga
Mwenyekiti
wa Chama cha ACT Wazalendo Mkoa wa Shinyanga Bi Siri Yassin amesema chama hicho kinatarajia kufanya Mkutano wa hadhara Mei 11, Mwaka huu
2023 Mjini Shinyanga.
Akizungumza
na Misalaba Blog Mwenyekiti huyo amesema Mkutano huo utafanyika katika uwanja
wa zimamoto eneo la Nguzonane kata ya Kambarage Mjini Shinyanga.
Amesema
viongozi wanaotarajiwa kuhudhuria ni pamoja na Mwenyekiti wa chama hicho Taifa
Bwana Zito Kabwe ambapo amewaomba wanachama pamoja na wananchi wengine wa Mkoa
wa Shinyanga kujitokeza kwa wingi kuhudhuria mkutano huo.
Bi.
Siri Yasin amesema kabla ya Mkutano huo viongozi pamoja na wanachama wa chama
hicho watashiriki shughuli za kijamii ikiwemo kupanda miti,na kuchangia damu
salama.
Post a Comment