" DAWA ZA BINADAMU ZENYE THAMANI YA SH.MILLION 43 ZAKAMATWA TABORA .

DAWA ZA BINADAMU ZENYE THAMANI YA SH.MILLION 43 ZAKAMATWA TABORA .

Na Lucas Raphael - Misalaba Blog,Tabora

 

Mamlaka ya dawa  na vifaa tiba  TMDA  kanda ya Magharibi  imekamata  dawa za binadamu na kuziondoa  katika  maduka ya dawa muhimu   zikiwa na thamani ya shilingi milioni 43 zilizokuwa zinauzwa kwa kificho kinyume maelekezo ya serikali.

 

Akizungumza na waandishi wa habari ofisini kwake  kaimu meneja wa  TMDA  kanda ya magharibi  Kiboko Magigi alisema kwamba  dawa zilizokamatwa  silikuwa hazipaswi kuunzwa kwenye maduka  dawa muhimu.

 

Alisema kwamba msako wa kukamata dawa hizo  ulifayika  katika  mkoa wa Tabora ,Katavi na Kigoma   nakuongeza kuwa  dawa hizo hazina madhara  kwa matumizi ya  binadamu .

 

Kiboko alisema kwamba kukamatwa kwa dawa hizo kunatokana na  kukiukwa kwa  kanuni ya 63 ya makundi ya dawa inayo zuia dawa hizo kuuzwa katika  maduka muhimu ya dawa.

 

Aidha kaimu meneja wa  TMDA  kanda ya magharibi  kwa mamlaka waliyopewa wanatakiwa kusambaza dawa hizo kwa vituo vywa watu wenye uhitaji ikiwemo Magereza ambako wanawafungwa ambao wanaea kutuia dawa hizo.

 

Alisema kwamba dawa hizo  imezikabidhiwa kwa jeshi la Magereza mkoani Tabora kwa ajili ya kuwapatia wafungwa ambapo  zitawasaida  matibabu wafungwa ambao wako  katika  gereza kuu la Uyui

Akipokea Dawa hizo Kaimu  mkuu wa Gereza kuu la Uyui Dkt.Richard  Malifedha aliishukuru Mamlaka ya dawa  na vifaa tiba  TMDA  kanda ya Magharibi  kwa kutoa dawa hizo kwa zahanati ya Gereza hilo hilo.

 

Alisema kwamba dawa hizo zitakuwa  ni msaada  mkubwa kwa wafungwa kutokana na uhaba wa dawa ambao umekuwa ukiwakabili mara kwa mara .

Alisema kwamba Gereza hilo linawihitaji wa dawa mbalimbali kwa ajili ya kuwasaidia wafungwa waliomo  ndani ya grezea kuu la uyui.

Kaimu meneja wa  TMDA  kanda ya magharibi  Kiboko Magigi aliyevaa suti ya Bluu akishuhudia ushushaji wa mabox ya madawa ya aina mbalimbali kwenye eneo la Magereza mkuu wa Uyui na kushuhudiwa na Askari wa vyeo mbalimbali wa jeshi la Magereza wakiongozwa na Kaimu mkuu wa Gereza hilo  Dkt Richard Malifedha .

Post a Comment

Previous Post Next Post