Na
Mwandishi wetu, Misalaba Blog
Umoja
wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi (UVCCM)
Mkoa wa Shinyanga umeendesha mafunzo ya darasa la
itikadi kwa vyuo vya kati na vyuo vikuu vilivyopo mkoa wa shinyanga kwa kipindi
cha siku nne kuanzia Aprili 26,2023 na kuhitimishwa Aprili 28,2023 lengo ni
kuwajenga vijana kujitegemea, kujitambua, kujua faida na hasara ya utandawazi,
maadili na uongozi ambapo wanavyuo 479 wamepata mafunzo hayo
Akizungumza mgeni rasmi katika kilele cha mafunzo hayo Mjumbe wa baraza Kuu la umoja wa vijana wa Chama Cha Mapinduzi UVCCM taifa Mkoa wa shinyanga Monalisa Faustine Daniel amewaasa wana chuo hao kuepuka kujiingeza kwenye makundi mabaya, kuwa na nidhamu pamoja na kuheshimiana katika maisha ya kila siku.
Monalisa amewasisitiza kuwa wamoja na kushirikiana katika shughuli mbalimbali ambapo pia amewakumbusha kuzingatia maadili mema na kwa kuiga mfano wa viongozi wazuri katika Taifa la Tanzania akiwemo Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan.
Mgeni rasmi huyo Monalisa amewakumbusha pia kumshirikisha Mungu katika mambo mbalimbali ya maisha yao na kwamba waweze kuepukana na mambo maovu.
"Tumtangulize mungu kwa kika Jambo tumuombe mungu atusaidie kuepuka makundi na mikumbo pamoja na tuwe na msimamo, huwezi ukawa kuongozi bora kama huna msimamo" amesema Monalisa Mjumbe Faustine Mjumbe wa Baraza kuu taifa mkoa wa shinyanga”.amesema Monalisa
Akizungumza mlezi wa umoja wa Chama cha Mapinduzi UVCCM chuo cha Ualimu SHYCOM Raphael Saimoni amesema miongoni mwa kozi zilizotolewa ni pamoja na Dhana ya kujitambua, Dhana ya utandawazi, Elimu ya kujitambua, Uongozi na Maadili, pamoja na Thamani ya kijana katika taifa kwa vyuo na vyuo vikuu mkoani shinyanga kwa lengo likiwa ni kuwajenga vijana kua Viongozi bora wa taifa la kesho.
Nao baadhi ya washiriki wa mafunzo hayo Wameushukuru uongozi wa Umoja wa vijana wa Chama cha Mapinduzi UVCCM Mkoa wa Shinyanga kuleta mafunzo hayo ambapo wamesema kutokana na mafunzo hayo wameimarika, na wako tayari kulitumikia taifa huku wengine wakisema kutokana na nafunzo hayo ya siku nne 04 tumeweza kujithamini
"Kutokana na mafunzo haya yametujengea kujiamini na kujitambu tupo tayari kulitetea naifa na chama cha mapinduzi kwa ujumla" Amesema masunga Dotto mshiriki wa mafunzo hayo.
"Tutumie vizuri mitandao ya kijamii tusitumie kwa kuangalia picha ambazo hazina maadili hali inayochochea ongezeko la kushiriki mapenzi ya jinsia moja ambapo ni kinyume cha maadili yetu ya kitanzania tutumie vizuri mitandao ya kijamii kwa manufaa ta kizazi kijacho" amesema Mery Faustini mshiriki wa mafunzo hayo

Mlezi wa umoja wa
Chama cha Mapinduzi UVCCM chuo cha Ualimu SHYCOM Raphael Saimoni akizungumza
kwenye mafunzo hayo

Post a Comment