CHAMA cha Alliance for Democratic Change (ADC) kanda ya nyanda za juu kusini kimeshauri wabunge kutunga sheria kali itakayokomesha vitendo vya ushoga na ndoa za jinsia moja hapa Nchini.
Huku kikiwataka mawaziri waliotajwa kuhusika na ubadhilifu wa fedha za umma kujiuzulu nafasi zao ili kupisha uchunguzi ufanyike kama sehemu ya kumsaidia Rais Dkt Samia Suluhu Hassan katika kuliongoza Taifa bila ya ufisadil.
Akizungumza leo katika kipindi cha Press leo kinachorushwa na chanel ya matukio Daima Tv kamishna wa ADC kanda ya nyanda za juu kusini Daus Masasi alisema kuwa pamoja na mambo mazuri yanayofanywa na serikali iliyopo madarakani chini ya Rais Dkt Samia Suluhu Hassan ila yapo mambo ya makwazo na kilio kikubwa kwa Taifa kama janga la Ushoga ,Usagaji na ndoa za jinsi moja ambalo mwarubaini wake ni wabunge kutunga sheria kali itakayokomesha vitendo hivyo .
“ Hawa wabunge wasilalamike kama tunavyolalamika sisi wananchi maana wao ndio wenye nafasi kubwa ya kukomesha tatizo hili kwa kulitungia sheria kali ambazo zitaliepusha Taifa na janga hili sasa kama wabunge hao wanalalamika nani atalifanyia kazi hili “
Alisema kuwa lazima wabunge kusimama kwa pamoja kupinga suala hili la ndoa za jinsia moja kwa kulitungia sheria kali kama ambavyo bunge la Uganda na serikali yake ilivyopitisha sheria kali ya ushoga na ndoa za jinsia moja .
Masasi alisema ripoti ya Dkt Harrison Mwakyembe imetaja wazi wazi mashirika ambayo yamekuwa yakihamasisha vitendo vya ushoga lakini mashirika hayo wizara ya afya inayatambua na ndio ambayo inayasimamia sasa ni vizuri wizara kuchukua hatua za haraka ili kulinusuru Taifa na janga hilo kubwa .
Pamoja na kutaka wabunge na wizara ya afya kuchukua hatua kulinda Taifa bado alishauri kumbi za starehe kuanza kufuatiliwa kwa karibu ili kuwakamata na kuwachukulia hatua za kisheria wale wote wanaojihusisha na uhamasishaji wa vitendo visivyo na maadili kwa Taifa .
Katika hatua nyingine Masasi alipongeza ripoti ya CAG kwa kuonesha mapungufu katika usimamizi wa fedha za miradi ya maendeleo na kuwa wote waliohusika na mapungufu hayo wanapaswa kumsaidia Rais Dkt Samia kwa kukaa pembeni ili kuruhusu uchunguzi ufanyike na ikibainika wamehusika katika ulaji wa fedha za umma basi sheria zichukuliwe dhidi yao pasipo kujali nafasi za uongozi walizokuwa wakizitumikia .
Pia wabunge kuacha unafiki katika suala la ripoti ya CAG maana wengi wao wanachuki binafsi na baadhi yao walipata kuwa mawaziri ila leo ndio wakosoaji wakubwa wa serikali .
Kuwa suala la wizi wa fedha za umma halijaanza leo bali lilikuwepo miaka yote isipo kuwa kipindi hiki cha Rais Dkt Samia kumekuwepo uwazi mkubwa wa utoaji wa taarifa ya CAG.
Alisema kuwa kupitia fedha zilizopotea kwa wachache kuzembea katika usimamizi kulikuwa na uwezekano wa Watanzania kupata huduma za afya kwa gharama ya fedha hizo za umma.
Aidha Masasi alimshauri Rais Dkt Samia katika teuzi zake mbali mbali za wabunge na wakuu wa wilaya na mikoa kutoa nafasi kwa watu kutoka vyema vya upinzani ili kuongeza nguvu ya usimamizi wa fedha za umma na kuisaidia serikali katika utendaji kazi wake .
Alisema kuwa tofauti ya Rais Dkt Samia na wengine waliotangulia ni moja kubwa ambapo Dkt Samia amekuwa akitanguliza huruma ya mama katika kuwahudumia watanzania huku mchwa wachache wameendelea kumkwamischa ndoto zake za kulitumikia Taifa .
Post a Comment