" DISMAS LYASSA APITISHWA NA KAMATI YA UTEKELEZAJI UVCCM KIBAHA MJINI KUWANOA VIJANA WILAYA

DISMAS LYASSA APITISHWA NA KAMATI YA UTEKELEZAJI UVCCM KIBAHA MJINI KUWANOA VIJANA WILAYA



MWANDISHI wa Habari mkongwe na Mtaalam wa masuala ya Uongozi na Utawala, ndugu Dismas Lyassa (kulia) amepitishwa rasmi na kamati ya utekelezaji Umoja wa Vijana wa CCM Wilaya Kibaha Mjini kusaidia kuwanoa vijana wa wilaya hiyo. 

 Akizungumza katika kikao maalum, Mwenyekiti wa UVCCM Wilaya ya Kibaha Mjini, Ramadhan Kazembe anasema wilaya imejipanga kuhakikisha vijana wananolewa vizuri katika nyanja mbalimbali. UVCCM wilaya imekuja na mkakati wa kuanzisha kamati nne; kamati ya Habari, kamati ya fedha na uchumi, kamati ya maendeleo ya jamii na kamati ya hamasa, ambazo zitanolewa kisha zitashuka chini kwa maana ya kata na matawi kufanya jambo kama hilo.

Pia anasema Kazembe. “Tumekuwa tukihitaji wanoaji, bahati nzuri tunaye ndugu yetu Dismas Lyassa, nakupongeza kwa kukubali ombi letu la kuwanoa vijana….tumekuja na kauli mbiu ya Vijana… Utumishi na ubunifu… tunatamani kuona mabadiliko makubwa katika umoja wa vijana,” anasisitiza Kazembe na kuongeza pia kamati imewateua wakufunzi wengine wawili kusaidia katika suala hilo.

Post a Comment

Previous Post Next Post