Na Lubango Mleka - Misalaba Blog, Igunga.
MKUU wa Mkoa wa Tabora Dkt. Batilda Burian amewaonya
Walimu ambao watabainika kuwafanyia ukatili Wanafunzi ikiwa ni pamoja na
kufanya mapenzi na Wanafunzi wakike, kuwalawiti wanafunzi wa kiume na hata kwa
Walimu wa kike ambao watabainika kujihusisha na mapenzi ya jinsia moja
(usagaji).
Hayo ameyabinisha alipokuwa anazindua miradi ya maji
inayosimamiwa na Mamlaka ya Maji Mjini na Vijijini Wilaya ya Igunga (RUWASA)
ambayo yameendana sambamba na kilele cha maadhimisho ya miaka 59 ya Muungano wa
Tanzania.
“Nipende kuongea na wanafunzi na walimu ambao leo
mmekuja hapa katika uzinduzi huu wa miradi ya maji, hivi karibuni kumeibuka
janga kubwa katika nchi yetu la ushoga na usagaji, watoto wetu wa kiume
wamekuwa wakiingiliwa kinyume na maumbile na walimu na wengine kubakwa, hivyo
niwaombe wanafunzi wote ukiona mwalimu anakushikashika katika sehemu za makalio
kwa watoto wa kiume na kwa wakike pia toa taarifa kwa walimu wengine au mwambie
mzazi wako na hata viongozi wa vijiji,” alisema Dkt Balozi Buriani.
Aliendelea kusema kuwa, “Endapo mtu huyo anayekufanyia
ukatili akakutishia eti ntakuuwa au ukitoa siri utaona usisite kutoa taarifa
sawa, na endapo ikabainika kuwa mwalimu umefanya jambo hili nitakuwa wa kwanza
kumchapa viboko kabla hajafikishwa Polisi na kama mzazi nitaita makamanda
watamcharaza viboko, jambo hili linasikitisha sana nanyinyi wananchi wa
Imalililo msikubali jambo hili likatoke kwa watoto wenu au vijana wenu, toeni
taarifa kwa mtu mtakaye mbaini kufanya uovu huo.”
Aidha, Dkt Batilda, ameipongeza RUWASA wilaya ya
Igunga kwa kuendelea kusimamia vyema miradi ambayo wanaitekeleza, jambo ambalo
limeendelea kupunguza kero kwa wananchi wa vijijini kwa kukosa huduma ya maji
safi na salama kwa miaka mingi.
Kwa upande wake meneja wa RUWASA Igunga Mhadisi Marwa
Sebastian Muraza, akisoma taarifa ya miradi hiyo, amemshukuru Rais Dkt Samia
Hassan Suluhu kwa kuendelea kuipatia fedha za utekelezaji wa mairadi RUWASA na
kuahidi kuendelea kusimamia miradi hiyo kwa ubora zaidi na kwa wakati ili
kutatua changamoto ya ukosekanaji wa maji safi na salama kwa wananchi wa
vijijini, jambo ambalo litawaondolea magonjwa ya mlipoko kama vile homa ya
matumbo, kuhara damu, magonjwa ya ngozi na kipindupindu pamoja na hatari ya
kujeruhiwa na wanyama wakali kama vile fisi na tembo.
“Ndugu mgeni rasmi tunaomba utuzindulie hii leo miradi
yetu ya maji katika vijiji vya Imalilo, Matinje utanufausha wananchi 1,613,
Kinungu watanufaika jumla ya wananchi 4,554, Mangungu jumla ya wanufaika 2,797,
Mibuyumiwili na Itunduru wananchi ni 7,074 wamefikiwa na huduma ya maji, Ntigu
na kijiji cha Moyofuke ni jumla ya wanakijiji 40,013, kwa vijiji vya Ziba na
Igumila ni wananchi 4,846 watanufaika na maji haya." alisema
Mhandisi Muraza.
Alimalizia kwa kusema kuwa "mwisho ni
kijiji cha Buchenjegele na Matindje ambapo wananchi wa vijiji hi ni 7,054
watanufaika, miradi hii yote imekamilika kwa asilimia 100 na itasimamiwa na
jumuiya ya watumiamji (CBWSO) chini ya usimamizi wa wataalamu kutoka
RUWASA Igunga na tayari wananchi na jumuiya wameisha panga bei za uuzaji maji
haya kwa ndoo itagharim shilingi 100, miradi yote hii imegharimu kiasi cha
shilingi 2,347,690,023."
Nao baadhi ya madiwani wa kata zilizozinduliwa
miradi hii ya maji kwa jimbo la Manonga na Igunga mjini waliojitamburisha kwa
majina ya Joladi Milenge kata ya Kinungu, Hyasinta Ngassa kata ya Nguru
kwa niaba ya madiwani wenzao wamemshukuru Rais Dkt Samia, Mkuu wa Mkoa wa
Tabora Dkt Balozi Batilda Buriani, Mkuu wa wilaya ya Igunga Sauda Mtondoo,
watumishi wote wa RUWASA mkoa wakiongozwa na Mhandisi Hatari Kapufi, wabunge wa
jimbo la Manonga na Igunga mjini pamoja na viongozi wote wa vijiji kwa
kusimamia na kuitekeleza Ilani ya CCM kwa kusimamia miradi hii vyema.
Huku baadhi ya wananchi waliojitambulisha kwa majina
ya Jane Luhenda, Grace Elias,Habiba Hamis, Bernadeta Shija na Stephan Jelemia
wamepongeza serikali kwa kuwakumbuka na kuwafikishia maji safi na salama kwani
vijiji vyao tokea nchi ya Tanzania imepata uhuru hawa kuwa na huduma ya maji
safi na salama.
“ Nimefurahi sana leo kupata maji kwani wanafunzi wetu
walikuwa watolo shuleni kwa kufuata maji mabili mwanafunzi anaondika saa moja
asubu kufuata maji anarudu saa tisa macha hivyo kumfanya kukosa masomo, hata
ndoa zetu sasa zitakwenda kuimarika na kumaliza kabisa ukatili wa vipogo kwa
wanawake na mabinti kubakwa na hata saazingine watoto wa kiume kulawitiwa hivyo
sasa matukio haya yanakwenda kuisha hapa kijijini kwetu,” alisema Jane Luhende.
Post a Comment