Na Mbaruku Yusuph,Tanga.
Mufti na Sheikh Mkuu wa Tanzania Dr Abubakar Zubeir amezitaka Taasisi za Kislaam kuacha kulumbana badala yake waelekeze fikra zao kwenye maendeleo ya kijamii yatakayowasaidia Waislam na wasiokuwa waislam.
Kauli hiyo ameitoa wakati wa ghafla ya kongamano la maendeleo ya Waislaam Jijini Tanga ambalo limeandaliwa na Taasisi za kislaam za TAMPRO na TIDF kwa ajili ya ujenzi wa Hospitali yenye kufuata maadili ya dini hiyo.
Muft Zubeir alisema lazima waislamu wawe wamoja na kuachana na mtafaruku wa kitaasisi ambao hautakuwa na maslahi kwa waumini ambao wanategemea kupata maendeleo kupitia Taasisi hizo.

Aidha alisema kutokujitambua,kutobadilika na kuacha mazoea ndio chanzo kwa waislamu kutoendelea na kurudi chini kimaendeleo jambo ambalo lazima lifanyiwe kazi ili kukabiliana na changamoto zinazoikumba dini hiyo.
Alisema ni jambo kubwa linalofanywa na Taasisi hizo kwa kuanzisha ujenzi wa Hospitali maalum itakayotoa matibabu yatakayothamini hadhi ya mwanamke wa kislaam na hata wasiokuwa waislamu kitu ambacho hakipo na kitakuwa mfano kwa Nchi nzima.
"Kwa sasa katika Hospitali zetu utakuta mwanamke wa dini zote anatibiwa na daktari mwanaume hasa maswala ya uzazi hii sio sahihi lakini inafanyika kutokana na kutokuwa na huduma hiyo"Alisema Muft Mkuu.
Mufti huyo alizidi kusema kuwa waislamu walipoteza dira baada ya kutokuwatumia wataalamu toka sekta mbalimbali ambao fikra zao zingeweza kujenga misingi bora kwa Taasisi za kiislaam na waumini wao kwa kuleta maendeleo badala ya kugombana wenyewe kwa wenyewe.
Hata hivyo alizitaka Taasisi hizo za TAMPRO na TIDF kutambua kwamba kila jambo linahitaji wataalamu ili kufanikishwa kwake na walitumie Baraza la Waislam Tanzania (bakwata) kutoa ushari na kukosoa kwa malengo ya kuleta maendeleo ya huduma za kijamii zitakazo wasaidia Waislaam na wasiokuwa Waislaam.
Awali akitoa taarifa fupi ya ujenzi wa Hospitali hiyo katibu wa Tampro Kombo Ramadhani alisema Hospitali hiyo kwa hatua ya awali itagharimu zaidi ya Shs bil 1.5 ambapo kutajengwa majengo saba ya ghorofa tatu ya kutolea huduma mbalimbali iliwemo watoto, kinamama,maabara,upasuaji,utawala na wodi za kinababa na dharura.
Ramadhani alisema lengo la kufanya kongamano hilo ni kuunganisha nguvu za waislaamu toka taasisi tofauti ili kuweza kutimiza azma ya ujenzi wa Hospitali hiyo itakayokuwa maalum kwa ajili ya kuangalia utu wa mwanaadamu.
"Tunatambua kuwa Bakwata ndio msimamizi wa Taasisi zote za kiislamu Nchini,tunakuomba Mufti utusimamie katika jambo hili ambalo ni la waislaamu wote Nchi nzima"Alisena Ramadhani.
Kwa upande wake muakilishi wa Mkuu wa Mkoa Tanga Kanali Maulid Hasan alisema jambo la mfumo wa dhana ya kujitegemea ni mpango mkakati na Serikali ipo tayari kutoa ushirikiano kwa Taasisi hizo ili kufikia malengo ya jitihada walizojiwekea
Kanali Hassan ambae poa ni Mkuu wa Wilaya Mkinga alisema kinachifanywa na Taasisi hizo ni mchango mkubwa wa kuisaidia Serikali kuongeza huduma za jamii kwa wananchi jambo ambalo labda lisingekuwa rahisi kufanywa na Serikaki.

Post a Comment