" SERIKALI YAWAKUMBUSHA WAZAZI JUU YA MALEZI BORA KWA WATOTO, SHIRIKA LA NANCY FOUNDATION LAENDELEZA MRADI WA HOME IS WHERE THE HEART IS”

SERIKALI YAWAKUMBUSHA WAZAZI JUU YA MALEZI BORA KWA WATOTO, SHIRIKA LA NANCY FOUNDATION LAENDELEZA MRADI WA HOME IS WHERE THE HEART IS”

Na Mapuli Misalaba, Shinyanga

Serikali Wilayani Shinyanga imewakumbusha wazazi na walezi kuwajibikia jukumu la malezi na makuzi bora kwa watoto ili kuandaa taifa lenye kizazi chenye maadili mema.

Kauli hiyo imetolewa na katibu tawala wa wilaya ya Shinyanga Bwana Boniphace Chambi kwenye hafla  iliyowakutanisha wazazi,walezi  na watoto wanaoishi katika mazingira magumu kwenye mitaa mbalimbali  Mjini Shinyanga,ambayo imeandaliwa na shirika lisilo la  kiserikali Nancy Foundation kwa kushirikiana na serikali.

Katibu tawala huyo amesisitiza wazazi na walezi kusimamia na kufuatilia mienendo ya watoto ili kudhibiti wasijihusishe na makundi yasiyofaa,ikiwa ni pamoja na kuwapatia mahitaji  yote ya msingi ikiwemo haki elimu.

“Ukimlea vizuri mtoto wako ipo siku atakuja kuwa wa msaada sana kwako kwahiyo wewe muombe mwenyezi Mungu jikusanye kusanye kwa chochote unachoweza kupata ili hatimaye mtoto umfikishe kwenye hatua furani sisi akina mama lazima tuone uchungu na tuone haja ya kuwalea watoto wetu”

“Lakini serikali haiwezi kuwaacha akina Baba waendelee kukataa watoto kuna namna ya kumshurutisha atoe matunzo kwa mtoto kwahiyo mama hakikisha unatoa taarifa kuna madawati ya njinsia ili serikali iweze kumchukulia hatua”.amesema Bwana Chambi

Mkurugenzi wa Shirika la Nancy Foundation Bwana Erza Manjerenga ameeleza hatua mbalimbali zilizofikiwa na mradi huo ambao umelenga kuwaokoa watoto wanaoishi na kufanya kazi mitaani katika Manispaa ya Shinyanga.

“Leo tulikuwa na kikao cha wazazi peke yao kuweza kujua sasa wao wanasema nini kuhusu changamoto zilizobainishwa na watoto wao lakini nao wazazi wamezungumza changamoto zao ikiwemo kukosa ada za wanafunzi, ugumu wa maisha na changamoto zingine hatua inayofuata ni kuhakikisha tunazifanyia kazi hizi changamoto zao zote tayari tumehakikisha kuwaunga na bima ya afya ambayo inatolewa na serikali CHF iliyoboreshwa ili wazazi hawa wawe salama wakazi wa magonjwa, maradhi katika familia yao lakini kingine ni kuona namna ya kusaidia kama vifaa vya shule”.

“Changamoto tuliyokutana nayo ni wazazi kushiriki wa kike wazazi wa kiume hakuna hata mmoja tunatamani sana kuona wazazi wa jinsia zate mwanaume na mwanamke wanashiriki pamoja ili tuweze kutatua changamoto hizi kwa uharaka watoto watimize ndoto zao”.amesema Mkurugenzi Manjerenga

Baadhi ya wazazi na walezi wa watoto wanaoishi mitaani wameahidi kushirikiana na shirika hilo pamoja na  serikali katika juhudi za kuwaondoa watoto hao kwenye mazingira hatarishi ya mitaani.

Mashirika mawili yasiyokuwa ya kiserikali Mkoani Shinyanga Nancy Foundation na Ubongo learing yanatekeleza  mradi wa kupunguza au kumaliza tatizo la watoto wanaoishi na kufanya kazi mtaani, mradi huo unaoitwa  “Home is where the heart is” .

 

Katibu tawala wa wilaya ya Shinyanga Bwana Boniphace Chambi akitoa elimu kwa baadhi ya watoto wanaoishi na kufanya kazi mitaani katika Manispaa ya Shinyanga.


Katibu tawala wa wilaya ya Shinyanga Bwana Boniphace Chambi akisisitiza mambo mbalimbali ya muhimu kwa wazazi wa watoto wanaoishi na kufanya kazi mitaani.

Katibu tawala wa wilaya ya Shinyanga Bwana Boniphace Chambi akisisitiza mambo mbalimbali ya muhimu kwa wazazi wa watoto wanaoishi na kufanya kazi mitaani.


Mwezeshaji kutoa polisi dawati la jinsia ambaye pia ni polisi wa kata ya Mjini Shinyanga ALINSP Jane Mwazembe akiendelea na zoezi la kuwapa chakula watoto wanaoishi na kufanya kazi mitaani katika Manispaa ya Shinyanga.


Katibu tawala wa wilaya ya Shinyanga Bwana Boniphace Chambi upande wa kushoto, Mwenyekiti wa mtaa wa Miti mirefu Bwana Nassor Warioba katikati na Mkurugenzi wa Shirika la Nancy Foundation Bwana Erza Manjerenga upande wa kulia wakiwa katika mazungumzo ya pamoja

Post a Comment

Previous Post Next Post