" SHEIKH WA MKOA WA SHINYANGA ISMAIL MAKUSANYA AZINDUA MSIKITI MPYA ULIOJENGWA NA JAI

SHEIKH WA MKOA WA SHINYANGA ISMAIL MAKUSANYA AZINDUA MSIKITI MPYA ULIOJENGWA NA JAI


Sheikh wa Mkoa wa Shinyanga, Ismail Makusanya, akikata utepe ikiwa ni sehemu ya kuzindua Msikiti mpya unaoitwa Masjid Walidayn, uliopo katika mtaa wa Majengo Mapya, kata ya Kitangili, Manispaa ya Shinyanga leo Mei 9, 2025.


Na Mapuli Kitina Misalaba

Sheikh wa Mkoa wa Shinyanga, Ismail Makusanya, amezindua rasmi Msikiti mpya unaoitwa Masjid Walidayn, uliopo katika mtaa wa Majengo Mapya, kata ya Kitangili, Manispaa ya Shinyanga.

Msikiti huo umejengwa na taasisi isiyo ya kiserikali JAMIIYAATULI AKHLAAQUL ISLAAM (JAI) kwa gharama ya Shilingi Milioni 50 hadi kukamilika, ambapo uzinduzi wake umefanyika leo Mei 9, 2025 baada ya Swala ya Ijumaa na kuhudhuriwa na waumini pamoja na viongozi mbalimbali wa dini na kijamii.

Akizungumza katika hafla hiyo, Sheikh Makusanya ameipongeza JAI kwa kujitolea na kusogeza huduma za kiroho karibu na wananchi, akisema kuwa hatua hiyo ni mfano wa kuigwa na wadau wengine wa maendeleo.

"Ni muhimu kwa taasisi na watu binafsi kuendeleza moyo wa kujitolea kama ilivyofanywa na JAI, ili kuimarisha maendeleo ya dini na jamii kwa ujumla," amesema Sheikh Makusanya huku akisisitiza umoja na mshikamano katika kutekeleza shughuli za maendeleo.

Ameihakikishia JAI kuwa Mkoa wa Shinyanga uko tayari kushirikiana na taasisi hiyo katika kufanikisha malengo yake kwenye sekta ya dini na huduma za kijamii.

Kwa upande wake, Amili wa JAI Mkoa wa Shinyanga, Ahmed Breck Jezan, amesema kuwa jumuiya hiyo imejikita katika kutoa huduma kwa watu wasiojiweza bila kujali tofauti za kidini, kijinsia, kabila au rika.

"Majukumu yetu ni pamoja na kusaidia yatima, wajane, wagonjwa na watu walioko katika mazingira hatarishi, pamoja na kutoa misaada ya kibinadamu na kuhamasisha jamii kuhusu uadilifu," amesema Jezan.

Naye Amili wa JAI Wilaya ya Kishapu, Said Hassan, amesema JAI pia inahamasisha ushiriki wa jamii katika masuala ya afya, kuchangia damu, na kulinda mazingira kama njia ya kukuza ustawi wa jamii.

Katika risala iliyoandaliwa na uongozi wa JAI na kusomwa na Ustadh Abdallah Samiji, taasisi hiyo imedhamiria kuendeleza mshikamano na amani, kuunganisha familia za wagonjwa na kuwapatanisha watu waliokosana katika jamii.

Wakati huo huo, viongozi mbalimbali walioshiriki hafla hiyo akiwemo Mwenyekiti wa UVCCM Wilaya ya Shinyanga, Abdulaziz Said Sakala, wameipongeza JAI kwa kazi nzuri na kuhimiza jamii kushirikiana na taasisi hiyo kwa ajili ya manufaa ya pamoja.

Katibu wa JAI Mkoa wa Shinyanga, Ashraph Majaliwa, amewashukuru waumini na wadau waliounga mkono ujenzi huo na kushiriki hafla ya uzinduzi, huku akiishukuru serikali na mashirika mengine kwa ushirikiano wanaoendelea kuupata.

Sheikh wa Mkoa wa Shinyanga, Ismail Makusanya, akikata utepe ikiwa ni sehemu ya kuzindua Msikiti mpya unaoitwa Masjid Walidayn, uliopo katika mtaa wa Majengo Mapya, kata ya Kitangili, Manispaa ya Shinyanga leo Mei 9, 2025.

Sheikh wa Mkoa wa Shinyanga, Ismail Makusanya, akizungumza wakati wa kuzindua Msikiti mpya unaoitwa Masjid Walidayn, uliopo katika mtaa wa Majengo Mapya, kata ya Kitangili, Manispaa ya Shinyanga leo Mei 9, 2025.

Sheikh wa Mkoa wa Shinyanga, Ismail Makusanya, akizungumza wakati wa kuzindua Msikiti mpya unaoitwa Masjid Walidayn, uliopo katika mtaa wa Majengo Mapya, kata ya Kitangili, Manispaa ya Shinyanga leo Mei 9, 2025.

Sheikh wa Mkoa wa Shinyanga, Ismail Makusanya, akizungumza wakati wa kuzindua Msikiti mpya unaoitwa Masjid Walidayn, uliopo katika mtaa wa Majengo Mapya, kata ya Kitangili, Manispaa ya Shinyanga leo Mei 9, 2025.

Amili wa JAI Mkoa wa Shinyanga, Ahmed Breck Jezan, akizungumza wakati wa hafla ya kuzindua Msikiti mpya unaoitwa Masjid Walidayn, uliopo katika mtaa wa Majengo Mapya, kata ya Kitangili, Manispaa ya Shinyanga leo Mei 9, 2025.Amili wa JAI Mkoa wa Shinyanga, Ahmed Breck Jezan, akizungumza wakati wa hafla ya kuzindua Msikiti mpya unaoitwa Masjid Walidayn, uliopo katika mtaa wa Majengo Mapya, kata ya Kitangili, Manispaa ya Shinyanga leo Mei 9, 2025. 

Amili wa JAI Wilaya ya Kishapu, Said Hassan, akizungumza wakati wa hafla ya kuzindua Msikiti mpya unaoitwa Masjid Walidayn, uliopo katika mtaa wa Majengo Mapya, kata ya Kitangili, Manispaa ya Shinyanga leo Mei 9, 2025.

Waamini wakiwa kwenye hafla ya kuzindua Msikiti mpya unaoitwa Masjid Walidayn, uliopo katika mtaa wa Majengo Mapya, kata ya Kitangili, Manispaa ya Shinyanga leo Mei 9, 2025.




Mwenyekiti wa Mtaa wa Majengo mapya akizungumza.





Post a Comment

Previous Post Next Post