Wanakikundi cha Huruma ya Mungu kutoka Parokia za Shinyanga mjini na Ngokolo katika Jimbo Katoliki Shinyanga, wamekabidhi msaada wa vitu mbalimbali kwa wafungwa wa Gereza kuu la Shinyanga, ili kuwawezesha kusherekea sikuu ya Pasaka.
Kufuatia msaada huo, wafugwa hao wamewashukuru wanakikundi cha Huruma ya Mungu, kwa kuwakumbuka na kujali mahitaji waliyonayo na wamewaomba waendelee na moyo huo.
Kwa upande wake Mkuu wa Gereza la Shinyanga SSP.William Makwaya, amesema msaada huo umekuja wakati mwafaka ili kuwawezesha wafungwa wajisikie vizuri na kuungana na wenzao waliopo nje ya gereza katika kusherekea sikukuu ya Pasaka .
Vitu hivyo ni pamoja na Ng'ombe mmoja, mchele kilo 300, mafuta ya kupikia lita 20, sabuni, nyanya, sukari pamoja na taulo za kike, ambapo kwa mujibu wa Mwenyekiti wa kikundi hicho Bw. Polycarp Kimario, vyote vina thamani ya zaidi ya Shilingi Milioni moja la laki sita.
Post a Comment