" WADAU WA SOKA WAOMBWA KUIUNGA MKONO TIMU YA STAND UNITED FC YA MKOANI SHINYANGA

WADAU WA SOKA WAOMBWA KUIUNGA MKONO TIMU YA STAND UNITED FC YA MKOANI SHINYANGA

Wasanii na wadau wa soka waliotoka Mkoani Shinyanga na kwasasa wanaishi jijini Dar es salaam na mikoa ya jirani wanatakiwa kuiunga mkono kwa hali na mali timu ya soka ya stand united FC inayoshiriki hatua ya nane bora ya michuano ya ligi daraja la pili maarufu first league huko jijini Dar es salaam.

Wasanii hao wanaongozwa na Judith Wambura maarufu Lady JD.

 Stand united FC ya Mkoani Shinyanga imeanza leo katika kampeni yake ya kupanda ligi daraja la kwanza maarufu championship msimu wa 20232024 katika hatua ya nane bora ambayo imegawanywa katika makundi mawili ya A na B.

Stand united iko katika kundi A lenye timu za Lipuli FC ya iringa,cosmopolitan FC ya Dar es salaam,Alliance FC ya mwanza na Stand united FC.kila timu itacheza michezo mitatu ambapo mshindi wa kwanza kundi A atacheza na mshindi wa pili kundi B na mshindi wa kwanza kundi B atacheza na mshindi wa pili kundi A. 

Kundi B lina timu za Dar city fc, Tma FC, Rhino Rangers FC na African Lyon FC.

Stand united imeanza leo kuchanga karata zake Jumatatu April 24,2023 kwa kumenyana na Alliance FC na kwamba imepata ushindi wa magoli mawili (2 – 0) huku Jumatano tarehe 26 ikiteremka tena dimbani kuvaana na cosmopolitan fc saa moja jioni na kuhitimisha na Lipuli FC Jjumaa April 28,2023 saa 10 kamili jioni, michezo yote itapigwa katika dimba la Azam complex chamazi.

Chonde chonde wadau wote wa stand united FC toka stendi za mabasi Dar es salaam na maeneo jirani kumbukeni sapoti yenu ni muhimu ili kuisaidia timu hiyo kufanya vizuri.

Kila la kheri stand united FC maarufu chama la wana wazee wa yes,yes,yes.


Post a Comment

Previous Post Next Post