
Wasanii na wadau wa soka waliotoka Mkoani Shinyanga na
kwasasa wanaishi jijini Dar es salaam na mikoa ya jirani wanatakiwa kuiunga
mkono kwa hali na mali timu ya soka ya stand united FC inayoshiriki hatua ya
nane bora ya michuano ya ligi daraja la pili maarufu first league huko jijini Dar
es salaam.
Wasanii hao wanaongozwa na Judith Wambura maarufu Lady
JD.
Stand united FC
ya Mkoani Shinyanga imeanza leo katika kampeni yake ya kupanda ligi daraja la
kwanza maarufu championship msimu wa 20232024 katika hatua ya nane bora ambayo
imegawanywa katika makundi mawili ya A na B.
Stand united iko katika kundi A lenye timu za Lipuli
FC ya iringa,cosmopolitan FC ya Dar es salaam,Alliance FC ya mwanza na Stand
united FC.kila timu itacheza michezo mitatu ambapo mshindi wa kwanza kundi A atacheza
na mshindi wa pili kundi B na mshindi wa kwanza kundi B atacheza na mshindi wa
pili kundi A.
Kundi B lina timu za Dar city fc, Tma FC, Rhino
Rangers FC na African Lyon FC.
Stand united imeanza leo kuchanga karata zake Jumatatu
April 24,2023 kwa kumenyana na Alliance FC na kwamba imepata ushindi wa magoli
mawili (2 – 0) huku Jumatano tarehe 26 ikiteremka tena dimbani kuvaana na
cosmopolitan fc saa moja jioni na kuhitimisha na Lipuli FC Jjumaa April 28,2023
saa 10 kamili jioni, michezo yote itapigwa katika dimba la Azam complex chamazi.
Chonde chonde wadau wote wa stand united FC toka
stendi za mabasi Dar es salaam na maeneo jirani kumbukeni sapoti yenu ni muhimu
ili kuisaidia timu hiyo kufanya vizuri.
Kila la kheri stand united FC maarufu chama la wana
wazee wa yes,yes,yes.



Post a Comment