Na Mapuli Misalaba,
Shinyanga
Wafanya biashara wa Soko
la Ngokolo mitumbani katika Manispaa ya Shinyanga wamesema kuboreshwa kwa
miundombinu mbalimbali ikiwemo vyoo na soko itawasaidia kufanya shughuli zao
katika mazingira rafiki na salama.
Wameyasema hayo leo Ijumaa Aprili 28,2023 wakati
wakizungumza na Misalaba Blog ambapo wamesema kuwepo kwa mazingira mazuri
katika eneo la biashara ni hali inayovutia watejainawaongezea wateja.
Wameipongeza serikali ya
Halmashauri ya Manispaa ya Shinyanga chini ya Mkurugenzi Dkt. Jomaary Satura,
Mstahiki meya Mhe. Elias Ramadhan Masumbuko kwa kushirikiana na mbunge wa shinyanga mjini Mhe. Paschal
Patrobas katambi, kuboresha mazingira ambapo wamesema inawasaidia kuongeza
kipato katika biashara zao.
Kwa upande wake katibu wa
soko la Ngokolo mitumbani Charles Mtegeko amewasihi wananchi wakiwemo
wafanyabiashara wa soko hilo kutunza
miundombinu ya soko pamoja na choo hicho cha kisasa ili kufikia malengo
yaliyokusudiwa na serikali.
Manispaa ya Shinyanga imeendelea kuboresha na kujenga miundombinu ya vyoo na masoko katika maeneo mbalimbali ya kibiashara katika Halmashauri hiyo.
Post a Comment