Na Mapuli Misalaba, Shinyanga
Kamati ya utekelezaji jumuiya ya wazazi kupitia chama cha
mapinduzi CCM Wilaya ya Shinyanga mjini imeendelea na ziara zake ambapo leo imetembelea
na kukagua uhai wa jumuiya katika kata ya Chibe, Ndembezi pamoja na kata ya Old
Shinyanga zilizopo Manispaa ya Shinyanga.
Pamoja na mambo mengine kamati hiyo imetembelea na kukagua hatua
zilizofikiwa katika uboreshaji wa Zahanati ya Chibe ambapo viongozi wa jumuiya
ya wazazi Wilaya ya Shinyanga mjini wameshauri namna bora ya kutatua changamoto
mbalimbali zilizopo kwenye Zahanati hiyo.
Viongozi wa jumuiya ya wazazi Wilaya ya Shinyanga mjini wamezungumza
na jumuiya za wazazi kata ya Chibe, kata ya Ndembezi pamoja na kata ya Old
Shinyanga ambapo wamepokea changamoto mbalimbali zinazokwamisha maendeleo huku
wakitoa maelekezo na kuahidi baadhi ya changamoto kuzishughulikia ili
kuendeleza umoja wa jumuiya hiyo.
Katika ziara hiyo
Mwenyekiti wa jumuiya ya wazazi Wilaya ya Shinyanga mjini Bwana Fue Mrindoko amezisisitiza
jumuiya hizo kuanzisha miradi mbalimbali ya maendeleo itakayowanufaisha wao na
jumuiya kwa ujumla.
Mwenyekiti huyo Bwana Mrindoko ameziomba jumuiya hizo kuendelea
kushirikiana na viongozi mbalimbali wa chama pamoja na serikali katika shughuli
mbalimbali za maendeleo ili kuleta matokeo chanya kwenye jamii na Taifa kwa
ujumla.
Amewashukuru kwa kumwamini katika nafasi hiyo ya Mwenyekiti
jumuiya ya wazazi Wilaya ya Shinyanga mjini huku akiwahakikishia wanachama na
viongozi kwenye matawi yote kuwa ataendelea kushirikiana nao ili kufikia
malengo yaliyokusudiwa.
Aidha Mwenyekiti wa jumuiya ya wazazi Wilaya ya Shinyanga mjini
Bwana Fue Mrindoko ametumia nafasi hiyo kuwaasa wazazi kulea watoto kwa
kuzingatia mila na distiri za Nchi ili kuwaepusha na mmomonyoko wa maadili.
“Wazazi
tunawajibu wa kuwapa elimu watoto wetu juu ya mila na desturi za Nchi hii maana
siku hizi wapo wasanii wanaonekana kwenye TV mavazi yao niya aibu na
ukifuatilia utakuta wametoka kwenye familia ambayo yupo Baba na Mama sisi
jumuiya ya wazazi hatukubaliani na tabia hizo niwaombe wazazi tuwape elimu
watoto wetu ili waachane na mila za wengine wafuate mila zetu za Tanzania”.amesema
Mwenyekiti Mrindoko
Kwa upande wake katibu wa jumuiya ya wazazi Wilaya ya
Shinyanga mjini Bi. Doris Kibabi amewataka wazazi kutoshirikiana na watoto wao
juu ya mambo mbalimbali yasiyofaa katika jamii ambayo hupelekea vishawishi vibaya
hasa kwa watoto wa kike.
Katibu huyo pia
amesisitiza jumuiya kwenye kata kuendelea kuongeza na kusajiri wanachama wapya
huku akikemea makundi mabaya kwenye jumuiya za wazazi kata ya Chibe, Ndembezi
na jumuiya ya wazazi kata ya Old Shinyanga.
Naye mjumbe wa kamati ya utekelezaji jumuiya ya wazazi
Wilaya ya Shinyanga mjini Mhandisi James Jumbe amewakumbusha wazazi kuhakikisha
watoto wao wanapata elimu stahiki ambapo amesema hali hiyo itasaidia kuwaepusha
watoto kujiingiza kwenye makundi yasiyofaa ambayo hukwamisha mafanikio katika
maisha yao ya kila siku.
“Elimu
ndiyo kila kitu kwenye Dunia hii kwahiyo tunatakiwa tushirikiana na serikali
hasa sisi wazazi kwenye malezi tuhakikishe watoto wanasoma Rais mama Samia
anajitahidi sana kuboresha miundombinu ya mazingira ya shule ili watoto waweze
kusoma, watoto wakisoma watapata maarifa ya kujiajiri au kuajiriwa ili kuja
kusaidia familia kwahiyo usikate tamaa kumsomesha mtoto kwa sababu ya changamoto
ndogondogo utashindwa kupata msaada zaidi ukija kuzeeka”. Amesema
Mhandisi Jumbe
Kamati ya utekelezaji jumuiya ya wazazi imeambatana na
viongozi wengine akiwemo katibu wa mbunge jimbo la Shinyanga Bwana Samwel
Jackson ambapo kamati hiyo leo Jumamosi
Mei 13,2023 imetembelea miradi mbalimbali ya maendeleo pamoja na kukagua uhai wa
jumuiya katika kata ya Chibe, Ndembezi pamoja na kata ya Old Shinyanga zilizopo
Manispaa ya Shinyanga.
Mwenyekiti wa jumuiya ya wazazi Wilaya ya Shinyanga mjini Bwana
Fue Mrindoko akizungumza ikiwa ni sehemu ya ziara kutembelea na kukagua uhai wa jumuiya kwenye kata leo Jumamosi Mei 13,2023.
Katibu wa jumuiya ya wazazi Wilaya ya Shinyanga mjini Bi.
Doris Kibabi akizungumza kwenye kikao cha pamoja na viongozi mbalimbali
wakiwemo wa jumuiya ya wazazi kata ya Ndembezi Manispaa ya Shinyanga leo
Jumamosi Mei 13,2023.
Mjumbe wa kamati ya utekelezaji jumuiya ya wazazi
Wilaya ya Shinyanga mjini Mhandisi James Jumbe akizungumzia malezi bora kwa
watoto wakati wa ziara hiyo leo Jumamosi Mei 13,2023.
Viongozi na wanachama mbalimbali wakiwemo wa jumuiya
ya wazazi kata ya Ndembezi wakiwa kwenye kikao cha pamoja na kamati ya
utekelezaji jumuiya ya wazazi Wilaya ya Shinyanga mjini leo Jumamosi Mei
13,2023.

Doris Kibabi akizungumza na jumuiya ya wazazi kata ya Old Shinyanga leo Mei
13,2023.
Katibu wa jumuiya ya wazazi Wilaya ya Shinyanga mjini Bi.
Doris Kibabi akizungumza na jumuiya ya wazazi kata ya Old Shinyanga leo Mei
13,2023.
Mjumbe wa kamati ya utekelezaji jumuiya ya wazazi
Wilaya ya Shinyanga mjini Mhandisi James Jumbe akizungumza na jumuiya ya wazazi
kata ya Old Shinyanga leo Jumamosi Mei 13,2023.
Katibu wa jumuiya ya wazazi Wilaya ya Shinyanga mjini Bi.
Doris Kibabi akizungumza na jumuiya ya wazazi kata ya Old Shinyanga leo Mei
13,2023.
Katibu wa jumuiya ya wazazi Wilaya ya Shinyanga mjini Bi.
Doris Kibabi akizungumza na jumuiya ya wazazi kata ya Old Shinyanga leo Mei
13,2023.
Mwenyekiti wa jumuiya ya wazazi Wilaya ya Shinyanga mjini Bwana
Fue Mrindoko akizungumza na wanachama wa jumuiya ya wazazi kata ya Old
Shinyanga leo Jumamosi Mei 13,2023.
Post a Comment