" TANGAZO LA NAFASI YA KAZI - ANAHITAJIKA VIDEOGRAPHER + GRAPHIC DESIGNER

TANGAZO LA NAFASI YA KAZI - ANAHITAJIKA VIDEOGRAPHER + GRAPHIC DESIGNER


 TANGAZO LA NAFASI YA KAZI

Misalaba Media inawatangazia Watanzania wenye sifa na uwezo kuomba nafasi ya kazi ifuatayo:

VIDEOGRAPHER + GRAPHIC DESIGNER (NAFASI 1)

Sifa za Mwombaji

  • Awe na elimu ya Graphic Design au taaluma nyingine zinazofanana.
  • Awe na uwezo wa kupiga picha na kurekodi video zenye ubora.
  • Awe na uzoefu wa kuhariri video kwa kutumia programu kama Adobe Premiere Pro au nyingine zinazofanana.
  • Awe na uwezo wa kutengeneza mabango (posters), thumbnails, logos na kazi nyingine za Graphic Design kwa kutumia Adobe Photoshop au programu zinazofanana.
  • Awe mbunifu na mwenye nidhamu.
  • Awe tayari kufanya kazi ndani na nje ya Mkoa wa Shinyanga pale inapohitajika.
  • Uzoefu wa kufanya kazi kwenye taasisi ya habari au kampuni ya uzalishaji wa maudhui utakuwa ni faida ya ziada.

Jinsi ya Kutuma Maombi

Waombaji watume barua ya maombi pamoja na:

  • Wasifu binafsi (CV).
  • Nakala za vyeti vya taaluma.
  • Sampuli za kazi (Portfolio) au viungo vya kazi walizowahi kufanya (ikiwa vipo).

Maombi yote yatumwe kupitia barua pepe:
misalabamedia@gmail.com

Ofisi Kuu za Misalaba Media zipo Shinyanga Mjini, karibu na Stand ya Zamani.

Mawasiliano

Simu: +255 745 594 231

Mwisho wa Kutuma Maombi

Tarehe 30 Julai, 2026.

Post a Comment

Previous Post Next Post