" RAIS SAMIA AFANYA UTEUZI, UHAMISHO WA WAKUU WA MIKOA NA MAKATIBU TAWALA WA MIKOA

RAIS SAMIA AFANYA UTEUZI, UHAMISHO WA WAKUU WA MIKOA NA MAKATIBU TAWALA WA MIKOA

 

Rais Samia Suluhu Hassan, amefanya uteuzi na uhamisho wa wakuu wa mikoa na makatibu tawala wa mikoa, ikiwa ni sehemu ya mabadiliko katika uongozi wa mikoa nchini.

Katika mabadiliko hayo, Abubakar Mussa Kunenge amehamishwa kutoka Pwani na kuwa Mkuu wa Mkoa wa Songwe, akichukua nafasi ya Jabiri Omari Makame ambaye atapangiwa majukumu mengine. Beno Moris Malisa amehamishwa kutoka Mbeya kwenda Tabora, akichukua nafasi ya Paul Matiko Chacha, aliyeteuliwa kuwa Katibu wa NEC, Idara ya Oganaizesheni ya CCM.

Adam Kighoma Malima amehamishwa kutoka Morogoro kwenda Lindi, akichukua nafasi ya Zainab Telack aliyestaafu, huku Queen Cuthbert Sendiga akihamishwa kutoka Manyara kwenda Morogoro.

Kwa upande wa Makatibu Tawala wa Mikoa, Richard Marcellino Kayombo ameteuliwa kuwa Katibu Tawala wa Mkoa wa Pwani. Balandya Mayuganya Elikana amehamishwa Mwanza kwenda Mbeya, Dkt. Fatuma Ramadhan Mganga kutoka Singida kwenda Mwanza, Pili Hassan Mnyema kutoka Pwani kwenda Shinyanga na Rodrick Lazaro Mpogolo kutoka Mbeya kwenda Singida.

Uapisho wa Wakuu wa Mikoa na Makatibu Tawala wateule utafanyika kwa tarehe itakayopangwa baadaye.

Post a Comment

Previous Post Next Post